January 20, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameguswa baada ya kumuona mtoto mmoja aitwaye Mudathiri Salum katika runinga akiomba msaada wa matibabu kuto­kana na kusumbuliwa na ugonjwa ambao umesaba­bisha mwili wake kudhoofu viungo vyake vikishindwa kufanya kazi na kushindwa kuzungumza.

Zahera ameongea na kuamua kumtafuta na kumchangia dola 300(Sh.690,000).

Akizungumzia tukio hilo la kumchangia mtoto Mudathiri Zahera alisema kuwa tukio la mtoto huyo kuonyeshwa akiomba msaada na mama yake, aliliona akiwa katika kambi yao ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Mwadui, waliyokuwa wameiweka katika Hoteli ya Nefaland iliyopo Manzese Argentina jijini Dar es Salaam.

Muda huo alikuwa amekaa zake chumbani akitazama taarifa ya habari katika runinga moja hivyo, alijikuta akiguswa na habari hiyo ya mama mmoja ambaye alimuona akimuonyesha mwanaye huyo anayesumbuliwa na maradhi akiomba msaada hivyo akaamua kumtafuta na kumchangia.

“Siku ya tukio hilo nilikuwa kambini katika maandalizi ya mchezo wetu uliyopita dhidi ya Mwadui, ilikuwa jioni hivi natazama taarifa ya habari, ghafla ikatoka habari ya mtoto huyo ambaye alikuwa akionekana amebebwa na mama yake akiomba msaada wa matibabu, kusema kweli niliingiwa na huruma hivyo nikaanza kutafuta ni wapi nitampata ili niweze walau kumchangia japo kidogo nilichonacho.

“Huwezi kuamini wakati tukio lile linaonyeshwa sikuweza hata kukariri namba za kutumia msaada wangu zaidi nilishika jina la runinga iliyorusha habari hiyo hivyo nikalazimika kumwambia msaidizi wangu mmoja awasiliane na wahusika ili wamfikishie mchango wangu huo,” alisema Zahera

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic