February 23, 2019




MWENYEKITI wa Chama cha waamuzi Tanzania, Salum Chama amewataka viongozi wa timu kuacha tabia za kuwatupia mzigo wa lawama waamuzi pale timu zake zinaposhindwa kupata matokeo uwanjani.

Mzunguko wa pili timu nyingi zimekuwa zikitoa malalamiko yao kwa waamuzi kushindwa kumudu kufuata sheria 17 hali inayofanya washindwe kupata matokeo.

Chama amesema kuwa viongozi wengi wanashindwa kutambua kwamba waamuzi wanapewa semina na wanajua wajibu wao hali inayowafanya watafute sababu pale wanaposhindwa.

"Wengi wakishindwa kupata matokeo uwanjani wanakimbilia kuwapa lawama waamuzi, ila hilo sio sawa wanatakiwa waangalie wao huwa inakuaje pale ambapo wanapata matokeo? mbona wanakaa kimya, Chama huwa kinatoa adhabu kwa waamuzi wanaoshindwa kumudu mchezo.

"Kuna sababu ambazo zinawaponza washindwe kupata matokeo mbali na waamuzi ambazo ni pamoja na kambi, mishahara, chakula, pia kuwajenga kisaikolojia, mwamuzi anaweza kuchangia kiasi kidogo maana naye ni binadamu," amesema Chama.

Timu ambazo zilishusha lawama kwa waamuzi ni pamoja na Yanga baada ya kutoa sare na Coastal Union, Azam FC baada ya kutoa sare na Coastal Union, JKT Tanzania baada ya kupoteza mbele ya Alliance.

1 COMMENTS:

  1. Simba mpaka sasa juu yakuwa lilikataliwa bao safilao kwakisingizio cha kuzidi na kunyimwa penelti ya wazi, juu ya hivo Simba haikulalamika kwa kutambuwa marefa ni binaadamu na kazi yao ni ngumu sana na si ajabu hata kidogo kuwa huenda kosa likatendeka bila ya kuonekana na marefarii na hilo sio hapa Tanzania tu lakini kote duniani.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic