February 20, 2019


Aliyewahi kuwa Ofisa Habari wa klabu ya Yanga na sasa akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, amewataka wachezaji Mrisho Ngasa na Haruna Moshi 'Boban' kuachana na mpira ili wafanye majukumu mengine.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Muro amesema kwa umri waliofikia hivi sasa hawana zile amsha-amsha za zamani hivyo si wakati mwafaka kwao kuendelea na soka.

Ameeleza kuwa wachezaji hao wameshashuka kiwango na wanapooza morali ndani ya kikosi cha Yanga ambacho anaamini kinahitaji damu inayochemka ili kuendana na ushindani katika ligi.

Muro ambaye alikitumia kiti cha Usemaji Yanga kwa kupambana vilivyo na Haji Manara haswa kwa majigambo na maneno, ameutaka uongozi wa Yanga kuhakikisha inashajili wachezaji ambao wanaendana na Yanga.

"Ifikie hatua klabu iangalia wachezaji ambao wanaleta hamasa ndani ya timu, vema ikasajili ambao wanaweza kupambana kwa ari na nguvu zote, ukimtazama Ngassa na Boban hawa muda wao umeshaisha na ni vema wakafanya mambo mengine nje ya soka" alisema.

3 COMMENTS:

  1. AMESEMA KWELI LAKINI AJABU ETI HAO SISI NDIO TUMESAJILI KWENYE DIRISHA DOGO TUTAACHA KUPIGWA ? AFADHALI TUNAKUTANA TENA MWAKA UJAO 2020 PENGINE ZAHERA ATASAJILI YEYE SASA

    ReplyDelete
  2. Kwani huyo Bobani ni nani aliyemsajili?!, si amesajiliwa kwa mapendekezo ya Zahera jamani! Sababu zingine sio za Mungu, kama hiyo ni ya Shetani. Kiuumla usajili mlichemka kwenye dirisha kubwa baada ya ligi ya 2017/2018 kuisha. Na sio mlichemka kwa kushindwa kupata wachezaji wazuri, hapana; mlishindwa kukosa fedha za kusajili wachezaji wazuri.

    ReplyDelete
  3. HAWA AINA YA WASEMAJI WANATAKIWA KUONESHA VITENDO BADALA YA MANENO. TIMU HAINA FEDHA ANATARAJIA WACHEZAJI ANAOWATAKA WATOKE MBINGUNI?
    MPIRA SIO SIASA NI TAALUMA NA UWEKEZAJI SIASA INATAKA NGUVU YA MDOMO NA USHAWISHI PEKEE NDIO MAANA NI RAHISI KUAMINISHA WATU KUWA PAPAI NA KARANGA NI KITU KIMOJA NA WATU WAKAAMINI.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic