February 23, 2019


MABINGWA watetezi wa JKT Queens wamegoma kufanya usajili mpya kwenye dirisha dogo kutokana na uimara wa kikosi chao.

JKT Quenss ni vinara wa ligi ya wanawake maarufu kama Serengeti Lite Women's Premier League ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni mzunguko wa pili.

Kocha Mkuu, Ally Ally amesema kuwa hawajaamua kufanya usajili kutokana na ubora wa wachezaji walionao zaidi watawapandisha wachezaji wawili kutoka timu B.

"Hatujafanya usajili kwenye dirisha dogo kwani wachezji wetu wote wana uwezo ila tumewapandisha wachezaji wawili kutoka timu B." amesema Ally.

JKT Queens wanaongoza ligi wakiwa na pointi 33 wameshinda michezo yote 11 na wamefunga mabao 72 na kufungwa mabao 3 dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufungwa jumatatu ya tarehe 25 mwezi Februari.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic