February 23, 2019


UONGOZI wa timu ya Namungo, umetoa ahadi ya fedha kwa wachezaji wa timu hiyo iwapo watafanikiwa kuwafunga Yanga katika mchezo wa Kombe la FA.

Namungo inatarajiwa kucheza na Yanga kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Majaliwa uliopo Ruhangwa, mkoani Lindi katika mchezo wa mzunguko wa tano.

Mwenyekiti wa timu hiyo, Hassan Zidadu, alisema kuwa wamekuwa na kawaida ya kutoa motisha kwa wachezaji wao katika kila mchezo ambao utahitaji kufanyika hivyo ili kuweza kupata matokeo huku akisisitiza kuwaheshimu wapinzani wao.

“Sisi hii kwetu ni mechi muhimu kwa sababu kwanza tunachezea kwenye uwanja wa nyumbani lakini bado tunatambua ukubwa na uzoefu wa wapinzani wetu, japo tulishacheza nao mchezo wa kirafiki lakini hauwezi kuwa sababu.

“Suala la kutoa motisha kwa wachezaji wetu hilo lipo na katika mchezo huu naamini kama uongozi tutakaa na kuweza kujua tunatoa kiasi gani iwapo tutafanikiwa kushinda kwa sababu ni malengo yetu,” alisema Zidadu.

CHANZO: CHAMPIONI

4 COMMENTS:

  1. Namungo hawataki kuendelea kwenye mashindano bali kumfurahisha Simba!!!
    Utakuta aliyeandika huu utumbo analipwa.
    Pathetic.
    Reasoning ya kijinga haswa.

    ReplyDelete
  2. Saleh jembe mnapaswa kujua kuwa mnaweza kufanya kazi nzuri zaidi ya huu upuuzi mnaoandika.watu wanataka kazi nzuri na sio pumba za unazi!You can do better than this nonsense!

    ReplyDelete
  3. Kwahiyo mashujaa nao waliwatoa simba kuifurahisha yanga ?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic