February 23, 2019




BAADA ya kushinda michezo mitatu bila kuruhusu bao kwa mlinda mlango wa Simba, Aishi Manula, jana rekodi ya michezo dhidi ya Mwadui FC, Yanga na African Lyon ilitibuliwa.

Frank Domayo ambaye amekuwa ni super sub baada ya kuingia akichukua nafasi ya Joseph Mahundi alizima ndoto za Manula kuendeleza ubabe wake wa kukaa langoni bila kufungwa.

Dakika ya 81 baada ya mshambuliaji Donald Ngoma kumzungusha anavyopenda beki wa Simba, Paul Bukaba aliachia pasi murua iliyotua miguuni mwa Domayo bila ajizi aliachia shuti kali.

Shuti hilo ambalo lilimshangaza Manula na mashabiki wa Simba liligonga kwenye mstari wa goli likarejea ndani ya uwanja baada ya kugonga mwamba na likamshangaza Domayo kabla ya kukutana na Obrey Chirwa ambaye kichwa cheke kilipaa mawinguni.

Manula anafungwa baada ya kucheza mechi tatu mfululizo bila kufungwa ambazo ni sawa na dakika 280 kwenye ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic