February 20, 2019



KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema aligundua mapema kuhusu ubovu wa uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo Arusha hali iliyofanya abadili mbinu za kupata matokeo.

Simba iliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Lyon ikiwa ugenini, mabao mawili yalifungwa na John Bocco na Adam Salamba alitupia bao moja.

Aussems amesema hesabu ilikuwa kupata pointi tatu kwenye mchezo huo muhimu ili kujiweka kwenye mazingira mazuri.

"Tulijua kwamba tunacheza uwanja mgumu kwetu hali iliyofanya tubadili mbinu ya uchezaji wetu kidogo kwa kuanza kucheza mipira mirefu hali iliyosaidia tukaibuka na ushindi ni furaha kwetu," amesema Ausems.

Matokeo hayo yanaifanya Simba ikusanye jumla ya pointi 42 ikiwa imecheza michezo 17 ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo huku kinara akiwa ni Yanga mwenye pointi 58 akiwa amecheza michezo 24.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic