February 23, 2019


BAADA ya Mtibwa Sugar kukubali kufungwa bao 1-0 dhidi ya KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara hivi karibuni, kocha mkuu Zuber Katwila amesema watalipa kisasi leo kwenye FA.

Mtibwa Sugar mzunguko wa pili wamekuwa katika wakati mgumu kupata matokeo hali ambayo imeifanya iporomoke mpaka nafasi ya 17 kwenye msimamo ilihali mzunguko wa kwanza ilikuwa ndani ya timu tano bora.

Katwila amesema kuwa kuna mambo mengi kwenye mpira ambayo yanaikumba Mtibwa ila imani yake itasimama na kurejea kwenye ubora wake.

"Tumepoteza dhidi ya KMC mchezo wetu wa Ligi bado tutakutana nao kwenye FA hivyo wajipange kwa kuwa sisi ni mabingwa watetezi na nafasi tunayo tutawaziba mdomo.

"Tunashindwa kupata matokeo yetu kwenye michezo yetu hilo lipo wazi ila tumegundua tatizo letu na tunalifanyia kazi ili kurejea kwenye ubora, washambuliaji wangu wameshindwa kumalizia nafasi wanazotengeneza," amesema Katwila.

Leo Katwila ana mtihani mbele ya KMC mchezo wa FA utakaochezwa uwanja wa Chamazi baada ya kufanya mabadiliko ya uwanja wa Uhuru kutokana na kuwa na matumizi mengine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic