February 22, 2019


Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara leo kati ya Simba dhidi ya Azam FC, baadhi ya mashabiki wa wekundu wa Msimbazi wameahidi kumfukuzisha Kocha Hans van der Pluijm.

Shabiki na mwanachama mmoja ambaye anajulikana kwa jina la Ayoub Kawea, ameeleza kuwa mechi ya leo ndiyo itakuwa safari ya kwaheri kwa Pluijm.

Akizungumza kupitia Radio One, shabiki huyo anaamini kuwa Simba itapata matokeo na akieleza Azam hawana ubavu wa kuwazuia kwa chochote kile.

Aidha, ameongeza kuwa Simba inawaheshimu Azam ila kwa mchezo wa leo inabidi wawaasamehe tu kwakuwa wanahitaji alama tatu kuendelea kusaka mbio za ubingwa.

Simba na Azam zitakutana Uwanja wa Taifa saa 10 jioni leo ambapo mechi hiyo itakuwa LIVE kupitia Azam TV

7 COMMENTS:

  1. Na Plujin pia apewe haki yake sio tu kusema Azam ikishindwa na Simba afukuzwe. Ikiwa timu dhaifu wa kulaumiwa sio kocha tu kwasababu uwezo na wa wachezaji wa Azam hauwezi kulinganishwa na ule uwezo wa wachezaji wa Simba. Kikosi cha Simba kina mi kipana na nyota wa hali ya juu kwa kila upande zaidi ya kile cha Azam. Ili Kupata matokeo mazuri shuleni, mwalimu mzuri lazima apate wanafunzi wazuri na katika mpira vilevile kocha mzuri pia lazima apate wachezaji wa hali ya juu na upatikanaji wa wachezaji wa hali ya juu sio masulia ya kocha tu. Tunasema Zahera ni kocha mzuri, lakini jaribu kumkabidhi zile timu zinazokamata mkia, unafikiri atawapiga pamu wawe wamejaa kwasababu ubora mara nyingi unakywa wakuzaliwa nao halafu ndio inafata juhudi na mwalimu mzuri.

    ReplyDelete
  2. Ni kweli mia mia. Hebu kwa mfano watani wetu Yanga ambao wana kocha mzuri na kikosi kizuri lakini jee wangepambanishwa na Al Ahli ambayo sote tumeona na wala sio masihara kutokana na uwezo wa wachezaji wa Yanga ambao hivi juzi tu walifungwa na Mwadui wangeiweza mikiki ya Al Ahli ya Misr?


    ReplyDelete
  3. Mmeiweza nyie Simba mliofungwa na Mbao.

    ReplyDelete
  4. Simba haitakuwa rahisi kuifunga Azam fc kama wanavyofikiria. Timu nyingi ligi kuu zinapocheza na Simba zinakimbilia kwenda kuwadhibiti eneo la kiungo na mara nyingi Simba baada ya kudhibitiwa eneo kiungo wanaonekana kukosa mbinu mbadala au kocha wao huchukua muda kabla ya kufanya marekebisho na timu kama Azam yenye kocha mzoefu kama Pluijm Simba wanaweza kukutana na fadhaha wasioitarajia jioni ya leo pale taifa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mlishindwa nini kuikamata Simba hapo kwenye kiungo na kuifunga? Matokeo yake mkajaza viungo mia, na mkapigwa cha Nguruwe.

      Delete
    2. Hivi FT score board inasomekaje?

      Delete
  5. Simba sc wananafansi kubwa yankushinda mchezobwa leo kama watajituma na kufanya juhudi kwakua azam nao wapo vzurii na wanauwezo wa kufanya maamuz yatakayowafanya wapate matokeo kikubwa simba wasijiamini sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic