February 23, 2019




KOCHA Mkuu wa Singida United, Mserbia Dragan Popadic kwa kushirikiana na Dusan Momcilovic ambaye ni msaidizi, amesema kuwa kinachoiponza timu yake kushindwa kupata matokeo chanya ni ubutu wa safu yake ya ushambuliaji.

Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema Popadic anauzoefu na ligi ila anakwamishwa na safu yake ya ushambuliaji ambayo bado inajijenga kurejea kwenye ubora.

"Kwa sasa bado hatujawa na matokeo chanya kwenye michezo yetu kutokana na safu ya ushambuliaji kutokuwa kwenye ubora, hilo tayari benchi la ufundi limeona na linafanyia kazi kwa ukaribu.

"Tuna shiriki ligi na FA hesabu zetu ni kuona tunafanya vizuri na kurejea kwenye ushindani kama ambavyo mashabiki wanahitaji, kikubwa sapoti na tunajua leo tunacheza na Coastal Union tupo tayari," amesema Katemana.

Singida United msimu huu haijawa na matokeo mazuri kwani kwa sasa inashika nafasi ya 18 ikiwa imecheza michezo 25 imejikusanyia pointi 29, leo itakuwa uwanja wa Chamazi kumenyana na Coastal Union mchezo wa kombe la FA.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic