February 20, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa amewapa kazi wachezaji wake kushinda mchezo wao wa leo dhidi ya Mbao utakaochezwa uwanja wa CC Kirumba.

Maneno hayo ni sawa na kuwajaza upepo wachezaji hao ili leo waibuke na ushindi mbele ya Mbao FC.

Yanga watacheza na Mbao FC wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa watani wa jadi uliochezwa Uwanja wa Taifa kwa kufungwa bao 1-0.

Zahera amesema baada ya kupoteza mchezo wao mbele ya Simba aliwatuliza wachezaji na kuwataka wasiwe na presha kwa kupoteza mchezo mmoja kwani haina maana kwamba hawawezi kushinda tena.

"Wachezaji wangu walifanya kazi nzuri ila kosa moja liliigharimu timu, niliwaambia kwamba wamecheza vizuri wanatakiwa wasahau habari za matokeo mabaya kwenye kichwa chao tuendelea kusoga mbele.

"Mchezo wetu dhidi ya Mbao najua utakuwa mgumu ila nina imani tutashinda, kama tulifanikiwa kuwashinda mchezo wa kwanza tutashidwa nini mchezo wa marudio? hivyo tukifanikiwa kushinda tunakuwa tumeshinda nyumbani na ugenini," amesema Zahera.

Yanga ni kinara wa ligi akiwa na pointi 58 baada ya kucheza michezo 24 amepoteza michezo miwili pekee mpaka sasa. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic