February 23, 2019


Kuelekea mechi ya Kombe la Fa dhidi ya Namungo FC, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amewaonya wachezaji wake kuhakikisha hawafanyi mchezo kwenye kupute hicho.

Zahera ameeleza kuwa mashindano hayo yana umuhimu mkubwa zaidi kwakwe kwakuwa anaweza kuisaidia Yanga kushiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kocha huyo amewapiga mkwara wachezaji wake kwa kuwataka wawekeze nguvu zao zote kuelekea mechi hiyo ambayo ni muhimu zaidi kwao.

Amesema hakuna mchezaji anayepaswa kuonesha dharau na timu yoyote ambayo watapangwa nayo kwani mechi zote ni muhimu na zinapaswa kutiliwa maanani.

"Nimewaambia wachezaji wangu wanapaswa kuwekeza nguvu na akili zote kuelekea mechi dhidi ya Namungo, haya ni mashindano muhimu na tunapaswa kushinda mchezo, tunaweza kupata nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu" alisema.

3 COMMENTS:

  1. LAKINI KWELI MAANA KULE KWENYE UBINGWA HUYO JAMAA MWENYE KOMBE LAKE AMEANZA KULIKUMBATIA DALILI ATALITETEA TAJI LAKE

    ReplyDelete
  2. Na kweli, inabidi mpambane, bila hivyo mtahesabu msimu wa pili kushiriki kimataifa. Ubingwa wa Kombe la ligi wala msiutegemee. Mkichemka hapo tu kesho, nina imani mtaanza kufukuzana wenyewe kwa wenyewe, kocha ataonekana hafai, baadhi ya wachezaji watatupiwa lawama, mwisho mtashangaa hata kwenye ligi mnaishia kumaliza nafasi ya 5 au 6.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic