February 23, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo amesema kila siku atawapatia mbinu mpya washambuliaji wake, Heritier Makambo na Ibrahim Ajibu kwa lengo la kuiimarisha safu yake hiyo ili watupie zaidi.

Yanga inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 58 ikicheza michezo 24.

Hii ikiwa ni kabla ya mechi yake ya jana mbele ya Mbao FC katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Akizungumza na Spoti Xtra, Zahera amesema; 

“Nahitaji kukaa na washambuliaji wangu kufanya marekebisho mbalimbali, nimeona kuna mapungufu katika kikosi changu kwa kuwapa mbinu mbalimbali za kufunga.

“Ligi ni ngumu ina ushindani hivyo nahitaji kukifanyia kazi kikosi changu kwa kuwa wakati mwingine wanashindwa kufuata maagizo ninayoyatoa, tunahitaji kushinda katika mechi zilizobakia,” alisema Zahera

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic