April 18, 2019


KARIBU tena mpendwa msomaji wa safu hii uipendayo ya Usipojipanga Tunakupanga. Wiki iliyopita tulimleta staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye kwa muda mrefu amekuwa haoneshi hadharani kumsapoti baba yake, Abdul Juma.

Katika kipindi cha hivi karibuni, Baba Diamond alikuwa akilalamika kutopata msaada wowote kwa mwanaye huyo baada ya kuugua miguu na kufikia hatua mbaya.

Ishu iliyoibuka, mzee huyo aliingia studio na kuachia Wimbo wa Dudu la Yuyu ambao umetokea kuteka mitandao ya kijamii. Katika wimbo huo ulimfikia hadi Diamond ambapo alionesha kupendezwa nao na kumfagilia baba yake huyo kwa kumuita Big Lion akichomeka mashairi ya wimbo huo.

Diamond alienda mbali zaidi, akiwa katika ziara yake na wasanii wake wa WCB, wimbo huo ulikuwa ukipigwa mara kwa mara kuonesha kuwa hana tatizo na baba yake.

Haya hapa chini ni maoni ya mashabiki baada ya Diamond kuonesha kumkubali baba yake.

Mimi naona Diamond ameanza kujirudi kwa baba yake, haiwezekani afurahie wimbo alioutunga baba yake. Namshauri sasa asimsapoti kwenye wimbo tu bali aangalie afya na mahitaji muhimu ya baba yake amsaidie, asiishie kumwita Big Lion. Mama Esther – Uhindini street, Dar.

Mimi naona Diamond ameamua kujirudisha kwa baba yake, namshauri asiishie kumwita big lion ageuze upande wa pili wa shilingi kwa kumwona ni Mungu wa pili chini ya jua. Mrs Kitivo – Malindi.

Safi sana Diamond, baba ni baba japo hajakutunda. Whity – Moro.

Mimi naona Diamond kama hajielewi tu, hakuna mzazi asiyekosea siku zote. Amsaidii baba yake mpaka alalamike kwenye mitandao. Montay Boko.

Maoni yangu ni kuwa, Diamond atakuwa ameupenda wimbo ameona kuwa utampa point ndiyo maana baada ya baba yake kutoa wimbo huo ndio amemkubali kwa hiyo hapo hamna mapenzi ya dhati isipokuwa kuangalia pesa tu. Nasir – Mtwara.

Mimi naona huyu Diamond kama ametahayari baada ya kuona mzee wake naye kakaa kimya kwa kutompatiliza, hana ishu huyo, si amegoma kumsaidia baba yake wakati ana maradhi ya miguu? Huo urafiki unatoka wapi? Mama Beaty – Pangan.

Kweli wazazi wa kiume wanazingua kwani hata mimi mzee aliacha kunisapoti muda sana lakini Diamond amsamehe kwani ni baba yake na amsampoti kwa sanaa na kwa hali yake kivyovyote vile. Akumbuke kwenye maandiko kuna hadithi ya mwana mpotevu alimkosea baba yake lakini baba alisamehe. Alex Nguma – Mjumbe wa Bodi ya Chama cha Waigizaji mkoa wa Temeke.

Diamond usije ukawa umejisogeza kwa mzee kisa wimbo wake tu ili uupigie noti halafu baadaye uingie mitini, Mungu atakuadhibu. Mwasasu – Nyehunge.

My Dear Mondi nakupenda sana na kumsapoti baba yako umenifanya kuona uzuri wako zaidi. Utafka mbali sana. Eva aka Tamisha.

Hapa ninaamini ukaribu wa Diamond na baba yake unaanza kurudi taratibu ila wale wanaofosi ndiyo wanaharibu lakini mzee wake anajua kosa lake. Tujifunze mababa kupitia kwa Chibu (Diamond). – Musa – Vigwaza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic