April 18, 2019



NAPATA kizunguzungu kufikiria namna mwenendo wa ligi yetu ya Tanzania inavyokwenda kutokana na mfumo uliopo na maendeleo yake yanavyokwenda kwa kusuasua hali ambayo inanifanya nitulie kidogo.
Nimekuwa na kawaida moja kila siku asubuhi kutazama namna ligi ya wenzetu kule ambako mpira wetu tunataka kuupeleka na hapa tulipo huwa najiuliza tunakwama wapi.
Kinachonifanya nishindwe kuelewa vizuri ni namna mashindano yao kwa wenzetu yalivyo mengi lakini bado wanauwiano sawa wa mechi za kucheza na kama ni kutofautiana hapo utakuta ni mechi mbili ama tatu tena za lazima.
Sasa kwenye ligi yetu sasa ni lazima niwe na panaldo pembeni ili nikimaliza kupitia nitulie kidogo kwani mambo kwetu ni mengi na muda wenyewe si rafiki.
Mpaka sasa kuna timu zina viporo mpaka tisa nyingine tatu swali kubwa la msingi mipango ya ligi yetu inakwama wapi na sio tatizo la siku moja bali ni miaka nenda rudi hapa pana tatizo bodi ya ligi inabidi ishtuke.
Kwa mazingira haya ushindani unazidi kuwa mdogo tena ni kwa baadhi ya timu jambo ambalo linaua ushindani wa ligi na kufanya ligi iwe na matabaka.
Hebu fikiria kwa yule ambaye amecheza michezo 32 akikutana na yule mwenye michezo michache unadhani nini kitatokea kama sio kupasua tu kichwa hapo msomaji.
Inakuwa ngumu kuleta ushindani hasa baada ya timu kugundua kwamba hazina cha kupoteza endapo zitashinda ama zitapoteza maana tayari inaingia uwanjani akili ya ushindani ikiwa imepotea.
Labda kidogo kwa yule ambaye anatafuta nafasi ya kubaki ligi kuu anaweza kuonyesha ushindani ili atetee nafasi yake kubaki ndani ya ligi je kwa yule ambaye hana nafasi ya kubaki ligi atashindania nini?
Je yule ambaye anajua hata ashinde ama asishinde atabaki kwenye ligi na msimu ujao ataendelea kupambana, atafanya nini kucheza na timu ambayo ina nguvu na viporo vya kutosha, lazima ushindani utakufa taratibu.
Ili ligi inoge na ilete ladha yenyewe ni lazima timu zishindanie nafasi ya kwanza asiwepo mwenye kuimiliki kwa namna anavyotaka hii inaua ushindani hata kwa yule anayeongoza.
Kinara anajua kwamba hata kama ikitokea anashindwa kupata matokeo bado ataongoza ligi hivyo atacheza namna anavyojiskia naye pia hana cha kupoteza.
Ifike wakati Bodi ya Ligi kwa kushirikiana na viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania watazame namna bora itakayotuondolea haya yote ambayo naona ni madudu na yanatibua ligi yetu.
Mchezo mbaya na unaomaliza wachezaji wetu ni upangaji wa matokeo hasa kwa nyakati hizi za mwisho na lala salama kila mmoja anatafuta mbinu itakayomfanya apate kile anachokitaka hii si sawa ni lazima ifanyiwe kazi.
Kama tatizo ni mashindano ya kimataifa basi ratiba iwe rafiki na mpangilio mzima ufuatwe kama ambavyo inapangiliwa na kukubaliwa.
Ule mtindo wa kuua mechi kisa maandalizi ya timu fulani naona usipewe nafasi kwani unafanya kuwe na matabaka ya timu zinazopewa kipaumbele nyingine zinaonekana zinasindikiza tu.
Misimu huu ambao unakwenda lala salama tumeshuhudia ushindani mkubwa licha ya kutokuwa na wadhamini hili liwe somo kujipanga vema msimu ujao kuona tunavunja yale ambayo tumeshindwa kuyafanya msimu huu.
Rai yangu ni kwamba mipango makini na ratiba bora itaikuza ligi yetu na kufanya ushindani kuwa mkubwa kila siku tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo kila timu inafanya vile ambavyo inajiskia kubadili ratiba.
Kila kitu kinawezekana endapo mipango itaanza mapema hasa kwa sasa masuala ya wadhamini yalipaswa yawe yamewekwa wazi na timu ziambiwe mapema kama kinaeleweka ama mambo bado.
Yasije kutokea kama msimu huu timu zinategemea kupata sapoti kutoka kwa mdhamini ghafla zinapewa taarifa hakuna mdhamini hii haitakuwa sawa.

Kutoka Championi

8 COMMENTS:

  1. Anguko la Yanga,wanazi wao watasingizia ratiba ila mpira ni kazi ya hadharani.

    ReplyDelete
  2. We ulishaona ligi ya wapi team ina viporo 9... Hii sio ligi ni madudu

    ReplyDelete
  3. Hivi hawa wanaolalamikia viporo kama wangetumia michezo yao vizuri nani angehoji timu fulani kuwa na viporo vingi?

    ReplyDelete
  4. "hebu fikiria kwa yule ambaye amecheza michezo 32 akikutana na yule mwenye michezo michache unadhani nini kitatokea kama sio kupasua tu kichwa hapo msomaji"

    Hapa mwandishi haueleweki kabisa ...umeandika kama vile umelewa.Hivi viporo vya timu nyingine zinaiathiri vipi nyingine..

    Nadhani kama Simba naye mechi zake angekuwa anacheza kwa ushindi wa kubahatisha 1-0 au 2-1 au 3-2 na wakati mwingine anatoa sare au anafungwa kama ilivyo Yanga basi tungeweza tabiri katika hivyo viporo 8 kuna ambavyo atatoa safe au kufungwa..Lakini sio hivyo kwa Simba kwani katika mechi 10 zilizopita amekuwa akishinda tu...Na dalili zinaonyesha huenda atashinda zote...Sasa ndio hapo wimbo wa viporo viporo...Yanga sasa hivi hawana Sababu kama ni mamilioni walianza ingiza tangu mechi ya Simba...hamna njaa tena.Tatizo ni benchi LA ufundi..

    ReplyDelete
  5. Ligi ya Tanzania kwa mtu mwenye akili timamu awezi kujisumbua kuelewa kinachoendelea,hii ya msimu huu ni moja ya ligi za ovyo ambayo sijawai kuona Wala kusikia duniani,viporo 11 kwa akili tu ya kawaida uwezi kutetea utumbo wa namna iyo,nakumbuka msimu wa 2016/2017 yanga ilikuwa na viporo 4 Simba na manara wao wakagoma kucheza mechi ili yanga wacheze viporo vyao akisema ni dalili dhairi ya kupanga matokeo sasa manara uyo uyo ameufyata mdomo juu ya viporo 11 vya timu yake na mashabiki wao wanaunga mkono ujinga huo,timu inacheza mechi ikiwa imeshachungulia mwenzake ameshinda ngapi na yeye ashinde ngapi kwa namna yoyote ile! angalia timu zilizokuwa zinashiriki michuano ya kimataifa viporo vyao avizidi mechi 4 Kila nchi lakini kwa Tanzania ni dunia nyingine! Atuwezi kuwa tunalea viongozi wa ovyo wanaoendesha taasisi kubwa za soka kwa mahaba badala ya kuzingatia uweledi ndo maana timu zetu zitakuwa wasindikizaji miaka yote,ligi mbovu uzalisha timu mbovu!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yanga wenyewe kwa akili ya TIMAMU waliamua kuanza kucheza mechi 11 Dar.Na waliambiwa wanabeti vibaya kwani mzunguko wa pili ambao watakuwa wanachezea viwanja vya ugenini, sio rahisi kupata matokeo kwani hata vibonde hukaza wasishuke daraja..Ni kwa utashi wao wanacheza mechi hizo zote kwani kama ilivyokuwa kwa Simba wana sababu ya msingi ya kukataa hadi viporo vipungue.Sasa hivi wanacheza UTUMBO na ikichangiwa na kuchezea ugenini hawafanyi vizuri wanalaumu waamuzi..Sasa hata kama mechi ya mtibwa refa angekubali goli feki...hakuna msaada wa muhimu point moja ingemfikisha popote..Yanga anapaswa kushukuru viporo vimeisaidia Simba kupata matokeo na poin CAF na sasa Yanga itapanda ndege kwa kupitia mgongo wa Simba mwakani...Labda kama watashinda Azam FA Cup!

      Delete
  6. Hivi Kama yanga kwenye kombe la mapinduzi angeingia finalize asingekuwa na viporo au mashindano ya sportpesa asingetolewa mwanzoni asingekuwa na viporo udhaifu wa timu Yao hawataki kuusema wanatafuta vijisababu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic