April 18, 2019


MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya Ndanda FC, Vitalis Mayanga mwenye mabao 10 kwa sasa kwenye ligi amesema kuwa kikosi chao kipo tayari kutibua rekodi ya kocha wa muda wa Azam FC, Idd Cheche ambaye hajapoteza mchezo mpaka sasa, leo Uwanja wa Nagwanda sijaona.
Cheche ameiongoza Azam kushinda mbele ya Lyon alishinda 3-1, JKT alishinda mabao 6-1, Singida United mabao 4-0, Kagera Sugar alishinda mabao 2-0, Mbao 0-0 na mchezo wa mwisho alishinda mbele ya Mbeya City kwa bao 1-0 hali iliyofanya timu yake kujikusanyia pointi 66 baada ya kucheza michezo 31.
Mayanga amesema kuwa wanatambua ugumu uliopo kwa sasa kwenye ligi wamejiandaa vizuri kutibua rekodi ambazo zimewekwa na kocha wa Azam FC.

"Rekodi zimewekwa ili zivunjwe nasi tumejiaanda vema kuona tunapata matokeo chanya hasa ukizingatia tutakuwa nyumbani tuna nafasi kubwa ya kupata matokeo kikubwa ni kujiamini.
"Maelekezo ambayo tumeyapata mpaka sasa yanatufanya tuzidi kujiamini, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona namna tutakavyofanya na ikumbukwe kwamba kwenye mpira kila kitu kinawezekana," amesema Mayanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic