April 17, 2019

KIKOSI cha timu ya Vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, leo kimepoteza mchezo wake wa pili mbele ya Uganda kwa kuchapwa mabao 3-0 uwanja wa Taifa.

Michuano hii ya Afcon kwa vijana inafanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania huku mwakilishi wa Tanzania, Serengeti Boys kwa mara ya kwanza alianza kwa kuchapwa mabao 5-4 na Nigeria na leo amefungwa mabao 3-0 na Uganda.

Makosa ya safu ya ulinzi pamoja na umakini dhaifu wa mlinda mlango wa Serengeti Boys umezidi kuididmiza timu ya Serengeti Boys ambayo ipo kundi A ikishikilia mkia bila kujikusanyia pointi.

Kocha wa Serengeti Boys, Oscar Mirambo amesema kuwa ni matokeo mabaya ila wanatengeneza vijana kwa ajili ya manufaa ya Taifa wakati ujao.

Sasa Serengeti Boys wamebakiwa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Angola ili kujaribu bahati yao kama itawezekana kufuzu michuano hii endapo Nigeria atamyoosha kwa mabao mengi mpinzani wake Uganda, huku naye akitakiwa kumtwanga mabao mengi Angola.

Kwenye kundi A Nigeria imefuzu kushiriki kombe la Dunia kwa vijana litakalofanyika mwaka huu, Brazili baada ya kuibuka kidedea mbele ya Angola leo kwa ushindi wa bao 1-0.

2 COMMENTS:

  1. KOCHA TOKEA MWANZO TULIONA GOLIKIPA HAYUKO SAWA KWANINI HUJARIBU GOLIKIPA MWINGINE? TUPO KWENYE MASHINDANO UNATUAMBIA UNATENGENEZA VIJANA KWAAJILI YA TAIFA WAKATI UJAO? KWANI NIGERIA NA UGANDA WAO NI KWAAJILI YA LEO? TUACHE LUGHA YA KURIDHIKA KUFUNGWA TAFUTA SABABU REKEBISHA MAKOSA

    ReplyDelete
  2. TFF na waamuzi pia mnajenga imani kwa watanzania kuwa mnawaonea Yanga kwa kukataa magoli yao....ligi ya mwaka huu tutajionea mengi....nadhani katika ligi zote hii ya mwaka huu imetia fora!...kwa madudu....Simba kucheza mechi 7 ndani ya siku 17...hata Patrick Aussems amelizungumzia hili...kwakweli tunapoelekea kama nchi si pazuri....si ajabu hata Serengeti Boys kutolewa....yaani laana inaitafuna TFF.....

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic