April 18, 2019


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), juzi lilipangua ratiba ya mechi za jana Jumatano za Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Coastal Union ya Tanga na Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mechi hizo awali zilipangwa kuchezwa kuanzia saa 10:00 jioni, lakini sasa zitaanza saa 8:00 kutokana na kupisha mechi ya Serengeti Boys dhidi ya Uganda ya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Boniface Wambura, alisema kuwa, mechi hizo zote kwa pamoja zitachezwa saa 8:00 mchana badala ya saa 10:00 kama ilivyokuwa hapo awali.

Wambura alisema walifikia uamuzi huo ili kupisha mchezo huo wa Serengeti Boys na Uganda ambao ulichezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar majira ya saa 11:00 jioni.

“Kwa hiyo kutokana na hali hiyo, mechi zote hizo zitaanza saa 8:00 mchana badala ya saa 10:00 kama ilivyokuwa hapo awali. “Tayari timu zote tumeshazipatia taarifa kuhusiana na mechi hizo, ni matumaini yetu kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa,” alisema Wambura.

Kwa upande wa Yanga, mratibu wa timu hiyo, Hafi dh Saleh, amethibitisha kuhusiana na mabadiliko hayo huku akisema kikosi chao kipo tayari kwa kucheza mechi hiyo katika muda huo katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Wakati Yanga wakicheza Morogoro, Simba wao watacheza kwenye Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga dhidi ya wenyeji wao, Coastal Union.

1 COMMENTS:

  1. TFF NA BODI YA LIGI MMEHARIBU LIGI YA MWAKA HUU HATA DUNIA INAJUA KUWA HAKUNA LADHA TENA YA MECHI ZA LIGI KUU

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic