April 18, 2019


Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amefunguka kuwa katika mechi walizofungwa msimu huu idadi kubwa zimechangizwa na maamuzi mabovu ya marefa wa Ligi Kuu Tanzania Bara waliochezesha mechi zao. .

Zahera amesema endapo kungekuwa na haki katika michezo yao basi wangekuwa wamejihakikishia Ubingwa mpaka sasa.

"Unajua mimi nimezunguka nchi nyingi sana Afrika lakini sijawahi kuona maamuzi ya hovyo kama ya waamuzi wa Ligi ya Tanzania.

"Hakuna haki na kungekuwa na haki nina uhakika sasaivi tungekuwa tushajihakikishia ubingwa."

Mbali na hilo Zahera amesema kwasasa anajipanga kwenye michezo inayofuata ukiwemo wa Azam ili kuhakikisha anashinda mechi zote zilizosalia.

Aidha , Kocha huyo amesema atahakihakikisha anatwaa ubingwa wa Kombe la ASFC ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani.

5 COMMENTS:

  1. TFF INAMLEA HUYU ANASEMA OVYO SANA SASA ANAWALAUMU MAREFA KWENYE MECHI ZIPI AMBAZO YANGA KAONEWA? KWANI HAMUONI NJE MAKOCHA WASEMA OVYO WANAPIGWA FAINI KUBWA TU ILI IWE FUNDISHO? TFF ACHENI KUWA HIVYO MNAHARIBU MPIRA

    ReplyDelete
  2. Hata timu anazozifunga nazo hulalamikia waamuzi kuwa wanaipendelea yanga mfano mechi na alliance hata costal union uniiko Cha ninja ilikuwa ale umeme hivyo afunge mdomo

    ReplyDelete
  3. Na ile mechi ya kwanza na Simba okwi alikataliwa bao la wazi mbona alikaa kimya

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic