May 4, 2019

BAADA ya jana, Donald Ngoma kufunga bao la ushindi dakika ya 73 kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho uliochezwa uwanja wa Chamazi, Kocha wa Azam FC Idd Cheche amesema hana hofu na Lipuli wala Yanga.

Cheche amesema anatambua kwamba kila timu imejipanga kupata ushindi hivyo naye anaanza maandalizi kwa ajili ya timu zote mbili kwa wakati mmoja.

"Tumeshinda mchezo wetu ni jambo zuri sasa tunakwenda kujiandaa kwa ajili ya timu yoyote itakayopenya kwenye hatua ya fainali," amesema.

Azam FC anamsubiri mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Lipuli na Yanga, mchezo utakaochezwa kesho uwanja wa Samora fainali itachezwa mkoani Lindi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic