May 5, 2019


KOCHA wa Lipuli, Seleman Matola amesema kuwa anamgoja kwa hamu kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kesho ili uwanja wa Samora mchezo wa nusu fainali ya ili kombe la FA amuonyeshe kazi kwa vitendo uwanjani.

Mchezo wa mwisho wa Yanga kucheza na Lipuli msimu huu ambao ulikuwa ni wa ligi, Yanga ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 uwanja wa Samora hali iliyomfanya kocha mkuu wa Yanga Zahera kupania kulipa kisasi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa amemsikia Zahera akidai kwamba alibahatisha kufunga hivyo yeye haoni taabu kuskia, hivyo kesho kila kitu kitakuwa wazi.

"Anahitaji kucheza na mimi, amenipata, nipo tayari kucheza naye na nimejipanga kutafuta ushindi ukizingatia nitakuwa nyumbani, hapo lazima tupambane.

"Mchezo mmoja ukishinda unatinga hatua ya fainali hilo nimewaambia wachezaji wangu, wakati ambao tunapitia ni mgumu ila tunatakiwa kupambana kupata matokeo uwanjani hilo linawezekana, mashabiki wajitokeze kwa wingi," amesema.

Mshindi wa mchezo wa kesho atakutana na Azam FC kwenye fainali ya kombe la Shirikisho itakayochezwa Lindi.

2 COMMENTS:

  1. Fanya kweli Matola mfunge mdomo huyo zahera

    ReplyDelete
  2. Kuuusu mechi za logo Zahera leo kaanza kunyanyuwa mikono juu Kwa kutamka kuwa wao kuupata ubingwa ni kitu hana tanaa nacho

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic