May 4, 2019


LIPULI FC ya mkoani Iringa imejipanga kisawasawa kuhakikisha inawatuliza wapinzani wao, Yanga watakaokutana nao Mei 6, mwaka huu katika mchezo wa Kombe la FA.

Lipuli FC inatarajiwa kuikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Samora Iringa katika hatua ya nusu fainali.

Katibu Mkuu wa Lipuli FC, Julius Leo alisema wamekuwa wakikusanya fedha kwa ajili ya kujiandaa na mechi za ligi pamoja na FA kuhakikisha wachezaji wake hawana matatizo yoyote kuelekea mchezo huo kwa kuwapatia mishahara yao.

“Kuna harambee ambayo tumeifanya hivi karibuni lengo likiwa ni kukusanya fedha kwa ajili ya kuwapatia wachezaji wetu waweze kumaliza vizuri ligi ikiwa ni pamoja na kushinda mchezo wa FA kuhakikisha tunawalipa mishahara yao kabla ya mchezo huo kufi ka.

“Tunahitaji kusonga mbele zaidi kwa kushinda mechi hiyo ili kuweza kutinga hatua ya fainali,” alisema Leo.

Mbali na harambee hiyo, taarifa kutoka Iringa zinaeleza kuwa baadhi ya wanachama na mashabiki wa Simba wamejiandaa kwa ajili ya kutoa hamasa kubwa katika mchezo huo ili kuwapa wakati mgumu watani zao wa jadi Yanga.

Mashabiki na wanachama hao wameamua kufanya hivyo ili kuimuza zaidi Yanga isiendelee kushiriki mashindano yoyote ya kimataifa msimu ujao.

1 COMMENTS:

  1. sio kwa yanga hii tunakaba hadi nafasi ya kocha lazima akae kimya.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic