May 5, 2019


MENEJA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa mlinda mlango David de Gea atabaki kuwa namba moja na atakaa leo langoni watakapokuwa wanaikabili Huddersfield.
Mhsipania De Gea amekuwa akifanya makosa mengi ya kiufundi kwenye mechi za hivi karibuni na alikubali  kufungwa bao la kusawazishwa walipocheza na Chelsea Uwanja wa Old Trafford Jumapili na kugawana pointi moja moja. baada ya sare ya bao 1-1.
"David de Gea amefundishwa vema wiki hii na atakuwa tayari kuanza dhidi ya Huddersfield naamini atafanya vizuri kwani mlinda mlango namba mbili, Sergio Romero ana maumivu aliyoyapata wakati wa mazoezi siku ya alhamisi," amesema.
Kwenye michezo 123 aliyocheza De Gea ambaye ni mchezaji bora kwenye misimu minne kati ya mitano amefanya makosa matatu yaliyosababisha kufungwa magoli ya moja kwa moja, lakini mchezaji huyo amefanya makosa hayo tena katika mechi zake nne za mwisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic