May 4, 2019

RUVU Shooting jana ilizindua rasmi sera ya 'PapasaSquare' baada ya kuifunga mabao 3-1 JKT Tanzania mchezo uliochezwa Uwanja wa Mabatini.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa huo ni mwanzo mpya kwao na watapambana ili kuendelea kushinda mechi zao zilizobaki.

"Tumezinduka rasmi sasa sera yetu inaanza kufanya kazi, niliiwaambia wapinzani wangu JKT wajipange sisi ndio tunazindua ligi wakatubeza sasa walichokipata kinawatosha, huo ni mwanzo wa kupapasaSquare," amesema Bwire.

Mabao ya Ruvu yalifungwa na Mussa Said dk ya 48, Emmanuel Martin dk ya 59 na Fully Maganga dk ya 90 huku lile la JKT Tanzania likifungwa na Ismail Aidan dk ya 45.

 Ushindi huo unaifanya Ruvu kujinasua kutoka nafasi ya 19 mpaka nafasi ya 13 wakiwa na pointi 39, JKT Tanzania wakiwa nafasi ya 14 wote wamecheza michezo 34 wana pointi 39.


1 COMMENTS:

  1. JKT Tanzania steam zote walimalizia kwa Simba matokeo yake wamekwenda kuchemsha kwa Ruvu shooting.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic