May 5, 2019

MSHAMBULIAJI wa Mbao FC, Said Said amesema kuwa kilicho nyuma ya mafanikio yake ni ushirikiano uliopo ndani ya timu kiujumla.

Said jana alifunga bao lake la nane kwenye ligi wakati timu yake ikiibuka na pointi tatu Uwanja wa CCM Kirumba dhidi ya Ndanda FC baada ya kushinda bao 1-0.

Akizungumza na Saleh Jembe, JR amesema kuwa wamekuwa na ushirikiano mkubwa ndani ya timu hali inayofanya kila mmoja atimize majukumu yake.

"Kwangu mimi naona kikubwa kinachonifanya nifanye vizuri ni ushirikiano ambao naupata kutoka kwa wachezaji wenzangu ndani ya timu, licha ya kushinda bad kazi ni kubwa ya kufanya.

"Tumekuwa tukipambana kwa hali na mali kuata matokeo ila mwisho wa siku lengo letu limetimia nina imani tutaendelea kufanya vizuri kwa mechi zetu zinazofuata," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic