May 4, 2019


BAADA ya kupoteza mchezowake wa jana kwa kufungwa mabao 2-1 na Simba, Kocha Mkuu wa Mbeya City, Ramadhan Nswanzurimo amesema kuwa kinachoiponza Simba kupokea vichapo ikiwa nje kwenye mashindano ya kimataifa ni kubebwa na waamuzi ambao wanashindwa kutafsri sheria 17.

Nswanzurimo amesema kuwa hajaona uwezo wa kikosi cha Simba jana kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Sokoine Mbeya, kwani kwa kiasi kikubwa walitawala mpira mwanzo mwisho ila waamuzi wakawaponza.

"Unajua timu kubwa kama Simba imetoka kuwakilisha nchi michuano ya kimataifa, waamuzi wa hapa wanaibeba sana sasa wakitoka nje huko wanapokea vichapo kwa kuwa hakuna anayewajua, ili kuboresha ligi tunahitaji kumpata mshindi bora na halali na sio mshindi wa kuchaguliwa.

"Nimeumia sana kupoteza mchezo wangu ilihali nilistahili kushinda hii sio sawa siwezi kuwalaumu waamuzi moja kwa moja ila wanachangia kudumaza maendeleo ya mpira wetu, kuna umuhimu wa kufuata sheria na utaratibu ili kukuza soka letu," amesema.

Simba kwenye hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika haikushinda mchezo hata mmoja nje iliishia kupewa zigo la mabao na timu ya As Vita mabao 5-0, Al Ahly mabao 5-0 na JS Saoura mabao 2-0.

11 COMMENTS:

  1. walichezesha waamuzi wa Tanzania ndio wakawabeba hadi rob

    ReplyDelete
  2. wewe wacha malalamiko kwani upo nafasi yangapi simba kwa sasa sio daraja yako ,simba wamecheza na yanga mzungumko wa mazo wamenyimwa goal safi wanyimwa goal walipocheza na lipuli waamuzi ndio hao hao kama ni uzaifu sikwaushindi wa simba tu hata wao wanaminywa

    ReplyDelete
  3. Alifundish wap kw mafanikio anawex kujivunia . Anaiga manen ya yanga kuna timu alifundisha amefikisha hata makundi. Wanajisemea tu kufanananisha usingiz na kifo

    ReplyDelete
  4. Kocha umeongea ukweli kabisa na next time wanapigwa 10 had mbelekeo fc

    ReplyDelete
  5. mbona okwi alingushwa ndani ya 18 simba hakupewa penati?

    ReplyDelete
  6. Simba haikufeli Ila ni timu pekee iliyowahi kufika hatuwa robo fainali nayo Simba ikapewa gingers na kupandishwa daraja

    ReplyDelete
  7. Kwanini kila mnapofungwa mnataka kujifichia kwenye kivuli cha simba kubebwa. Jana napo yale magoli hayakuwa ya halali ama? au kuna mahala mlifungwa refa akaminya. Mfanye ujinga wenyewe kwa kujilinda na kukaribisha mashambulizi golini kwenu mpaka nacheza madhambi na sasa unakuja kuongea upuuzi ili uonewe huruma na kama ungekuwa na uwezo wa juu usingekuwa unashika nafasi ya mwishoni huko. Bora ukae kimya na kuiandaa timu yako kwa mechi zilizobakia ili usishuke daraja.

    ReplyDelete
  8. Anatafuta uchochoro wa kutokea asije akufukuzwa Mbeya city sio ile ya Juma Mwambusi
    Kwani timu yake imefungwa na Simba tu, raha mechi iko live kila mtu anaona, timu yake iliridhika na goli moja wakaanza kupoteza muda ni uzembe wao kwa mechi ya jana kwa hali ya uwanjani walikuwa wanashinda mchezo

    ReplyDelete
  9. Kocha huelewi unachokiongea, ivi kimataifa simba walifeli? Robo fainali ndo kufeli?

    ReplyDelete
  10. watanzania wenzangu naomba kujua mafanikio ya timu ni nini? kubeba kombe au kufika fainali nani mwenye mafanikio? tunaudumaza mpira wetu kwa kujisifu ujinga jaman hebu tubadilike

    ReplyDelete
  11. Huyu kocha boya kabisa hivi kufika robo fainali ni kufeli? Hakuna team kwa ukanda huu wa CECAFA iliyofanya hivyo hata vitimu vyao vya Burundi havijawahi wala havioti kufikia hatua hiyo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic