May 4, 2019


NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta anazidi kutakata kwenye Ligi Kuu ya Ubelgiji akiwa ni kinara wa utupiaji wa mabao ambapo mpaka sasa amefikisha jumla ya mabao 23.

Samatta anayekipiga Genk jana aliongeza bao lake la 23 wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Antwerp ikiwa ni mechi ya play off.

Anayemfuatia kwenye ufungaji katika Ligi hiyo ni mshambuliaji wa timu ya Zulte Waregem ambaye ni raia wa Tunisia mwenye mabao 18, Hamdi Harbaoui.

Genk kibindoni wamejikusanyia jumla ya pointi 50 wakifuatiwa na wapinzani wao wa karibu Club Brugge wenye pointi 41.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic