May 5, 2019



MSHAMBULIAJI namba moja kwenye Ligi Kuu ya England kwa kutupia mabao Mohamed Salah akiwa nayo 22 atakuwa fiti kumenyana na Barcelona mchezo wa marudio  Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaochezwa Jumanne.
Salah ambaye aliumia baada ya kugongana na mlinda mlango wa Newcastle, wakati wakishinda kwa mabao 3-2, Martin Dubravka  na kupata maumivu ya kichwa atakuwepo Jumanne, isipokuwa mshambuliaji mwenzake Roberto Firmino ataukosa mchezo huo.
Liverpool wanahitaji ushindi wa mabao zaidi ya 3-0 ili kutinga hatua ya fainali kwenye mchezo huo utakaochezwa uwanja wa Anfield baada ya kukubali kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 nusu fainali ya kwanza.
Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa Salah yupo sawa, alipata maumivu kwenye kichwa chake akapewa matibabu na alibaki uwanjani kushuhudia mchezo ukikamilika, akiwa kwenye chumba cha kubadilishia nguo.
"Daktari alikuwa na uwezo wa kufanya maamuzi atoe huduma wapi ndani ya uwanja ama nje ya uwanja, yeye alichagua nje ya uwanja na tumekubaliana na hayo.
"Tunatarajia kumkosa Firmino ambaye anasumbuliwa na matatizo ya misuli hivyo hatakuwa tayari kucheza Jumanne, labda mpaka Jumapili kwenye mchezo wetu dhidi ya Wolves," amesema.






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic