May 5, 2019


YANGA Leo Mei 5 wanaandika historia mpya kwa kuchagua viongozi wapya ambao wataiongoza timu hiyo kwa muda wa miaka minne.

Leo zoezi hilo linafanyika katika ukumbi wa bwalo la Polisi ambapo wagombea kwa nafasi zote walipata fursa ya kuzungumza sera zao na wanachama kupata fursa ya kuuliza maswali.

Nafasi ambazo zinagombewa ni ngazi tatu ya kwanza ni ngazi ya Mwenyekiti, ngazi ya pili ni ya Makamu Mwenyekiti na ngazi ya tatu ni ya Ujumbe wa Kamati Tendaji ndani ya Yanga.

Zoezi ambalo linaendelea kwa sasa ni upigaji kura ambapo matokeo yanatarajiwa kutangazwa saa 12:00 Jioni ya leo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic