June 22, 2019




TREZEGUET AKIWA NA SALAH

Wenyeji wa michuano ya Afcon, Misri wameanza michuano hiyo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimbabwe.

Mechi hiyo ya ufunguzi wa michuano ya Afcon kwenye Uwanja wa Taifa jijini Cairo, Misri walikwenda mapumziko wakiwa na bao 1-0, mfungaji akiwa Mohamed Trezeguet.

Hata hivyo, Khama Billiat wa Zimbabwe ndiye alikuwa msumbufu zaidi upande wa ngome ya Misri na wenyeji walilazimika kufanya kazi ya ziada kupata bao.


Zimbabwe walionekana kucheza kwa kujiamini lakini tatizo likawa ni mashambulizi dhaifu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic