June 20, 2019



Mwanachama na shabiki maarufu wa klabu ya Yanga, Rostam Aziz leo ametokea hadharani na kusema kswamba haungi mkono klabu yake kumilikiwa na mtu mmoja.

Rostam ameyasema hayo leo mchana wakati akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo na waandishi, Rostam amesema hakubaliani na suala la mtu mmoja kumiliki klabu hiyo au kufadhili, badala yake anaunga mkono udhamini.

“Mtu mmoja amiliki klabu kubwa kama Yanga, yenye wanachama mamilioni. Hili si sahihi, hata ufadhili ni nia ya mango wa nyuma kuimiliki klabu,” alisema.

“Kwangu binafsi nitaendelea kuisaidia Yanga kama shabiki na mwanachama. Kikubwa ni uongozi kuangalia namna ya kufanya mambo yaliyo sahihi lakini si umiliki kutoka kwa mtu mmoja.


“Yanga inaweza kuingiza fedha zake kupitia udhamini, matangazo ya runinga lakini pia suala la kuuza bidhaa zake kama jezi na kadhalika,” alisisitiza.

8 COMMENTS:

  1. Kwa wazo hilo hatutafika popote

    ReplyDelete
  2. Udhamini ndio mzuri kama vile Sportspesa

    ReplyDelete
  3. Klabu iwe na vyanzo vyake madhubuti na vya kudumu vya mapato vilivyodhibitiwa

    ReplyDelete
  4. hivi mtu akiwa na pesa ndio mwanachama maarufu

    ReplyDelete
  5. Nitumu gani yenye wanachama milioni,semeni washabiki na wapenzi.

    ReplyDelete
  6. Kuna haja kubwa kwa viongozi wa vilabu kukaa na kutafakari ni jinsi gani klabu inaweza kujiendesha kibiashara na kiuchumi kuliko hoja ya kumtegemea mfadhili kwa kuuza hisa kama walivyofanya Simba.Jambo la kwanza na muhimu kwa viongozi wa vilabu hasa hivi vikubwa 1.Kuhakiki wanachama wao wote waliokuwa hai na kuandikisha wapya wafanye kwenye mtindo wa kileo sio ule wa kizamani,2.kuhakisha bidhaa zao hasa zinye nembo ya klabu zisitapake hovyo ziwe na udhibiti wa hali ya juu ili klabu inufaike.3.Kuwe na maduka maalum yaliyosajiliwa na kutambulika na klabu kwa kuuza bidhaa zao hapo patakuwa na udhibiti wa kutosha.4.Michango ya uwanachama ikusanywe kwa utaratibu maalum kama haya yatandeka klabu ahazitahangaika hata siku moja

    ReplyDelete
  7. Mambo mawili katika maisha kama utashindwa kujimiliki basi bora umilikiwe kuliko kuwa Omba Omba.Kumilikiwa kwa mikataba yenye tija na manufaa kwa pamde zote mbili na kuwa omba omba mashuhuri bora nini? Sifa yakuwa na wanachama wengi hewa wasioweza hata kwenda uwanjani kuisapoti timu kuna faida gani? Kwani hujasikia TP MAZEMBE mmiliki wake katumbi lakini ni timu ya wananchi wa Lubumbashi? Hizi akili zetu za kitanzania zimejaa unafiki unaolea umasikini na unyonge. We unadhani Joto na vurugu la wanachama wa Liverpool au Chelsea nakuwa chini ya mmiliki ni wajinga? Basi kama timu inayomaliza kuuza ticket za misimu miwili ya ligi ya mbele ijayo inayokuja ni wajinga kuwa na mmiliki, na kuona timu zetu ambazo hata siku ya mechi watu hawajai uwanjani kuwa ni ujanja wa akili basi tujue watanzania akili zetu zinaburutwa na watu fulani wasioitakia nchi hii maendeleo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hao Chelsea wana hali gani kwa sasa? Jiulize Man U wana hali gani kwa sasa? Club imeshachukuliwa na mtu mmoja na matokeo yake wanachama hawana cha kwao!! Jiulize club kama Barca, RM, Arsenal nk mbona zinaendeshwa na wanachama na zinaperform? Hapa tatizo ni viongozi! Hivi leo Mo akifa au akaamua kuondoka hiyo Simba itakuwa na hali gani? Lazima tuangalie mbele badala ya kuangalia leo.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic