June 20, 2019




Simba imeamua kujiimarisha zaidi katika sehemu ya kiungo cha ukabaji kwa kuvuka mipaka hadi nchini Sudan ambako imemsajili kiungo Bora mara mbili mfululizo wa Ligi Kuu ya Sudan.

Huyo ni mchezaji wa timu ya taifa ya Sudan tangu akiwa na miaka 17 akitokea kwa mabingwa mara tatu mfululizo wa Ligi Kuu ya Sudan klabu ya Al Hilal.

 Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman amejiunga na Mabingwa wa nchi kwa mkataba wa mwaka mmoja, leo. 


King guys anajulikana kea pasi za uhakika lakini ukabaji wake wa nguvu na ubora wa upigaji mipira ya vichwa.


15 COMMENTS:

  1. kwann wasimpe mkataba wa mia 2 au zaid ndo tatizo la timu za bongo.

    ReplyDelete
  2. NAIONA SIMBA ya kisasa, usajiliunaendana na mapungufu ya timu, wenye professinalism ya mpira wanaelewa kinachoendelea. thank you mnyama.

    ReplyDelete
  3. Mwanamme kasafiri hewani kwa kimo ila Yanga nao utasikia wanasaini msudani khaa!

    ReplyDelete
  4. Atapewaje kandarasi ya miaka miwili mtu ashazeeka! Mkata upepo kazeeeeek, huyo ameletwa ale upepo sio kukata upepo. Hela zinawasumbua mtasajili hata vitumbua wenzenu walivyoviacha.

    ReplyDelete
  5. mnasifia baraza la wazee
    kilomon fc

    ReplyDelete
  6. ikiwa mtu mwenye miaka 25 ni mzee basi dunia imeisha

    ReplyDelete
  7. Wazee wanamambo bana ndokusema mmesahau kabisaa alichowafanya kagere-mzee

    ReplyDelete
  8. Ronaldo Mzee? Nyie vyura ushindani na Simba ni kama mnajitafutia majanga.yule Ngasa ni kababu kabisa..

    ReplyDelete
  9. Anatisha Msudani kazi ipo akikukanyaga umekwisha akikuangukia umekwisha na ukimuangukia Pia umekwisha

    ReplyDelete
  10. Kwa kuwa simjuwi basi yangu macho kazi yangu kukaa kimya ili nione je ana ubora au hana kitu maana simba sc ya sasa sio ya mchezo na majaribio!

    ReplyDelete
  11. Amezeeka hata Kagere, Okwi na Boko Pia mlisema wamezeeka na ndio walioamka na kutoa kamasi watu

    ReplyDelete
  12. Kagere mlikauka kumcheka mkasema shaibu aliezeeka

    ReplyDelete
  13. Simba kanogewa na klabu bingwa Africa na walishaanza kunitia hofu kwenye usajili wa msimu huu wa ligi lakini sasa nimeshaanza kuwaelewa.Hawa wanaume wanaowashusha hivi sasa inaonesha kweli Simba wameamua kujenga timu isiyozoeleka kuwepo kwenye ardhi ya Tanzania hilo halina ubishi wacha tutulie na kuendelea kufuatilia trailers mpaka mkanda nzima wa usajili wa Simba utakopokamilika. Lakini hakuna ubishi Simba wanatengeneza timu kubwa yenye wachezaji wa kazi kweli kweli inatisha kwa kweli si ajabu ukaona Yanga wanapangua usajili kwani Yanga wamesjili watoto wa shule wengi na kuja kuuchalenji ubingwa wa simba kwa msimu unaofuata ni ndoto za kuku kwenda kumfanyia vurugu kipanga hewani. Ila ninachowaomba Simba waachane na maneno maneno ya watu wanaoponda usajili wa Shamte wa Lipuli kwanza ni mchezaji wa Simba asilia anyway ni miongoni mwa wachezaji wa Simba waliondoka au kuondolewa au kuamua kuondoka Simba lakini walipokwenda au kupelekwa wakabakia kujitambua.Na nnaimani kama alivyo miraji Athumani, Shamte ni miongoni mwa wachezaji ambao wanajua nini shida ya kutokuwepo ndani ya kikosi cha Simba nnaimani hawatakuja kuzembea tena pale simba kwa hivyo Shamte ni bonge la usajili mimi huwa siropokwi kwa hivyo chonde chonde wakuu ili kuimarisha beki mbili Shamte atakuja kuwa bonge la msaada kwa Simba.kwa upande wachezaji wazawa waliopo ndani ya Simba naona wengi bado wamebweteka na sitoshangaa kuona Simba wakiwaondoa baadhi yao ila kama ingewezekana wakawacha ili kuwapa nafasi msimu huu kuwaangalia zaidi yawezekana wakapevuka kiakili kwani wachezaji wengi wa kitanzania tatizo sio uwezo wa mpira. Tatizo kubwa la Wachezaji wa kitanzania liko kunako akili. Waswahili wanaamini kwa mchimba kisima kila anapoyakaribia yakuta maji basi ndipo anapokutana na jiwe ngumu badala ya udongo.Na ili kuyapata maji basi mchimba kisima anatkiwa kuamua kupambana na jiwe na kuyafikia maji na kujineemesha yeye mwenyewe binafsi na umma unaomzunguka kwa neema ya maji kwa vizazi kazaa vijavyo au aamue kuachana na kupambana na mwamba wa jiwe baada ya kazi kubwa na ya ziada aliyokwishaifanya ya kuichokoza ardhi kutoka usawa wa dunia na kuifukua kwa ajili ya matarijio ya kumpatia maji.Nimetoa mifano huo nikilenga kwa undani zaidi ule unyonge wa akili na hali ya kukata tamaa mapema au kuridhika kwa wachezaji wa kitanzania hadi inakera wakiwa na umri mdogo na uwezo mzuri wa kimpira. Pale Simba kutokana na hali halisi ya kiuchumi ya nchi yetu wakati mwengine unaweza kusema klabu zetu kama vile zinajitolea kutoa huduma kwa Wachezaji wetu ili na wao angalau wawe na mawazo ya kujitoa kwa ajili ya timu zao lakini walahi si kwa vijana wetu. Si mkude si Dilunga,Ndemla,mzamiru,si mo Ibrahim au Rashid Juma na wengine wengi naamimi bado hawajaonesha kuwa Siria na kazi yao kwani kuwepo Simba sio kwamba ushayafikia maji na unaanza kubwetaka, hapana kazi ndio kwanza inaanza ya kupambana na jiwe ili utobowe zaidi. Kuna wachezaji watakosa ajira zao ndani ya Simba msimu huu na hakuna jengine isipokuwa ni uzembe.Mfano wakati kama huu kwa mchezaji mwenye kujitambua lazima atakuwa yupo vitani kujiweka fiti na hata timu zinapoanza kambi ya pre season yeye anakuwa anakwenda kupasha moto misuli yake tu kwani alishajiweka fiti zamani sana na hiyo ndio akili ya kumroga kocha ili akukubali na sio kwenda kwa mganga. Timu kama Simba mchezaji asitarajie kabisa kuwa na namba ya uhakika bila ya yeye mwenyewe binafsi kuwa mwamba wa uhakika ngangari gado la sivyo utaishia kuchoma mahindi kwenye benchi na kubakia kulalama na kutishia kuhamia Yanga wakati ukitoka Simba huukatakiwi kuwaza kwenda Yanga. Unatakiwa kuwaza kwenda mbali zaidi na hiyo ndio akili.

    ReplyDelete
  14. Acha tusajili tu simba si walituletea wenyewe kwenye majaribio yao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic