June 20, 2019


MAKAMU Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela,  leo Juni 20, 2019,  akiongea na wanahabari makao makuu ya klabu hiyo,  ametoa kauli kuhusu mchezaji Ibrahimu Ajibu, kwamba klabu hiyo inamtakia kila la heri popote anapotaka kwenda.

“Mkataba wake unamalizika mwisho wa mwezi huu, mazungumzo yamefanyika na klabu imempa nafasi ya kuamua kama anapenda kubaki nafasi ipo, lakini kama anataka kuondoka klabu inamtakia kila la kheri, ”  alisema Mwakalebela akizungumza na vyombo vya habari.

7 COMMENTS:

  1. Hatumtaki Ajibu lakini ile mi asist tutaimis saaana

    ReplyDelete
  2. Hili suala la Ajibu hebu liishe aachwe tu kama Kocha amependekeza aachwe hakuwa kwenye mpango wake....kwanini waandishi mnashabikia sana hili suala? Halafu huyo Kindoki mpelekeni kwa mkopo halafu badala yake msajili makipa waliopo stars (Kalambo na Metacha) muongezeni either beki wa kushoto Erick Rutanga au Kiungo mkabaji kutoka Asante Kotoko kutoka Ghana...mchezo uishe

    ReplyDelete
  3. Sasa Nani asiyemtaka mwenzie Ajibu haitaki Yanga au Yanga ndio isiyomtaka Ajibu? Leo hatakiwi lakini kesho anafatwa Mzee wake. Kisebusebu na kiroho Pappo na huku Zahera anasema anamtaka na kesho hayupo katika ajenda yake

    ReplyDelete
  4. Kwani Yanga mnamlazimisha asaini mkataba wenu? Ajibu sio wa thamani waliyoitoa TP Mazembe au kwa mishahara ya kuchagiza..Kajiendee Simba hao ndiyo wamekulea na kukufundisha soka...Namba ni ngumu lakini akibadilika na kufanya bidii atafanikiwa zaidi Simba...akileta za Mkude hatafika popote!

    ReplyDelete
  5. Linalowaumiza Yanga ni Kumuona Ajibu anarejea alipozaliwa na kulelewa Jambo ambalo haliingii akilini hata kidogo. Vipi Yanga wanatumia Neno kuwa Ajibu akitaka kuondoka ruhsa Ambae mchezaji si wao na aibu kumnganganiya na huku mchezaji akionesha kila dalili kuwa hataki kubaki. Yanga si wanaamini kuipiku Simba na kuwafanyia umafia Kwa kuwanyanganya wachezaji walioletwa na Simba ikawa leo wanalalama kujiona Mateka na huku Mr Ten eti akiicheka Simba kwakuwa Hakuna usajili WA mana

    ReplyDelete
  6. Nimekupenda Makamu Mwenyekiti umesema ukweli kuhusu Ajib. Ni mchezaji mzuri lakini kusema ukweli hana dalili za kubaki Yanga.

    ReplyDelete
  7. Nini maanaake yanga kuiraihishia Simba kumsajili Ajibu wakati mchezaji si wa yanga tena. Mwachieni kwasababu angekuwa anatutaka angelikwisha zamani kukubaliana na asingetupiga chenga na kuzima simu ni lazima tuwe na ari kwani Yanga ni taasisi kubwa yenye kuheshimika Kote duniani. Kama hatutaki mara moja nasi tusimtake mara kumi na huo ndio uungwana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic