ASANTE Kwasi aliyekuwa beki wa zamani wa Mbao FC na Simba kwa sasa yupo kwenye hesabu za kutua ndani ya kikosi chake cha zamani Lipuli.
Ofisa Habari wa Lipuli, Clement Sanga amesema kuwa hakuna tatizo kwa Kwasi kurejea ndani ya kikosi hicho endapo ataona inampendeza.
"Lipuli ni klabu bora ambayo haibagui wachezaji wenye uwezo ama wale ambao wanaona ni sehemu sahihi kwao, kwa sasa hatuna tatizo na Kwasi anakaribishwa nyumbani.
"Aliondoka bila ugomvi nasi tulimpa baraka zetu hivyo kwa sasa tunaangalia kama anaweza kupata nafasi ya kusajiliwa," amesema.
Kwasi ametemwa na klabu ya Simba kutokana na kushindwa kuwika msimu wake wa pili kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya goti.

0 COMMENTS:
Post a Comment