KUMEKUCHA leo vita nyingine ya nusu fainali kwenye michuano ya Afcon inayoendelea nchini Misri ni kati ya Nigeria dhidi ya Algeria utakaopigwa majira ya saa 4:00 usiku uwanja wa kimataifa wa Cairo.
Timu zote zimejipanga kiasi cha kutosha kutinga hatua ya fainali hivyo mchezo wa leo hautakuwa na wepesi hata kidogo.
Wapinzani hawa tayari wameshawahi kumenyana mara nane kwenye michuano ya Afcon ambayo wenyeji Misri nao watakuwa wakiwatazama tu jamaa wakitamba kwenye ardhi yao ya nyumbani.
Rekodi zinaonyesha kwamba Nigeria wameibamiza Algeria mara nne huku wapinzani Algeria ambao waliibamiza Tanzania mabao 3-0 wao wakiibuka na ushindi mara tatu mbele ya Nigeria huku mechi moja wakitoshana nguvu.
Ni moja kati ya mchezo utakaovuta hisia za wengi hasa ukizingatia kwamba Nigeria wao waliwatoa kimasomaso wababe wa Misri ambao ni Afrika Kusini.
nyie waandishi hampo makini tatizo mnaandika habari za kukurupuka hata hamna wahariri wa kuangalia mlichokiandika, badilikeni bhana
ReplyDeletenao ni bnadamu
ReplyDelete