MICHUANO ya Afcon bado inazidi kunoga ambapo kwa sasa ni hatua ya nusu fainali na Senegal itamenyana na Tunisia ni miongoni mwa mechi tamu na ngumu.
Rekodi zinaonyesha kwamba mpaka sasa tayari Senegal na Tunisia zimemenyana mara tano kwenye michuano ya Afcon hivyo leo ni vita ya kisasi.
Kwenye mechi zote hizo tano hakuna mbabe kwani walitoka sare mara tatu huku kila mmoja akiibuka na ushindi mechi moja moja hiyo ilikuwa ni kuanzaia mwaka 1965 tena wakakutana mwaka 2002 mwaka 2004 ilikuwa ni robo fainali na Tunisia waliibamiza Senegal bao 1-0, 2008 hatua ya makundi ngoma ikawa sare ya mabao 2-2.
Senegal ambao waliibamiza mabao 2-0 Tanzania walilipa kisasi mwaka 2017 kwa kuibamiza mabao 2-0 Tunisia kwenye hatua ya makundi hivyo leo ngoma itakuwa nzito kwenye mchezo wa leo utakaopigwa nchini Misri.
0 COMMENTS:
Post a Comment