UONGOZI wa
Azam FC umesema kuwa kuelekea kwenye mchezo wa marudio dhidi ya Fasil Kenema ya
Ethiopia umejipanga kulipa kisasi ukiwa nyumbani Jumamosi ya wiki hii Uwanja
wa Chamazi.
Azam FC
mchezo wa awali nchini Ethiopia ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0, kwa
sasa inahitaji ushindi kwenye mchezo wa marudio ili kusonga mbele ili wakutane
na mshindi wa mchezo kati ya Triangle FC ya Zimbabwe ama Rukinzo ya Burundi na
itaanzia nyumbani kati ya Septemba 13-15.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa kikosi kimeanza maandalizi kwa
ajili ya mchezo huo.
“Tayari
Kocha Ettienne Ndayiragije ameanza kuwapa program maalumu vijana kwa ajili ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo wetu wa marudio tuna imani ya kufanya
vizuri kwani tutakuwa nyumbani.
“Uwanja wa
Chamazi hakuna kinachoshindikana kwani wachezaji wanautambua vema uwanja na
morali ya kusonga mbele kwenye michuano hii mikubwa Afrika upo juu, mashabiki
wajitokeze kwa wingi,” amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment