August 22, 2019



 PATRICK Aussems, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa ana imani na kikosi chake kitapata ushindi mbele ya wapinzani wao UD do Songo kwenye mchezo wa marudio utakaochezwa Agosti 25 uwanja wa Taifa.

Simba ililazimisha suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa uliochezwa uwanja wa Beira, nchini Msumbiji.

Akizungumza na Saleh Jembe, Aussems amesema ana imani kubwa na kikosi chake kupata ushindi kwenye mchezo wa marudio.

“Kikubwa ninachoshukuru ni kwamba hatujaruhusu bao tulipkuwa ugenini sasa kazi yetu imebaki kutafuta ushindi mbele ya wapinzani wetu.

“Ambacho kinanipa matumaini ni nguvu ya mashabiki wa Simba pamoja na uzuri wa uwanja wa nyumbani, hakuna namna nyingine tutakayofanya zaidi ya kutafuta matokeo.” Amesema Aussems.

3 COMMENTS:

  1. Ujumbe umefika nasi tutaujaza uwanja kutetea heshima ya Tanzania na Simba yenyewe na tunamuomba Mungu awe nasi pamoja timu zote za nyumbani zinazoshiriki mechi hizi za kitaifa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic