August 22, 2019


JACKSON Mayanja, Kocha Mkuu wa KMC amesema kuwa kikosi kipo imara kwa ajili ya mchezo wao wa kesho dhidi ya AS Kigali utakaochezwa uwanja wa Taifa.

KMC kesho ina kibarua mbele ya AS Kigali ya Rwanda kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho baada ya ule wa awali kutoshana nguvu kwa kutoka sare ya bila kufungana.

Akizungumza na Saleh Jembe,  Mayanja amesema mchezo utakuwa wa wazi na wamejipanga kupata matokeo chanya licha ya kutokuwa na washambuliaji halisi.

"Kuna baadhi ya majeruhi ambao wapo kwetu jambo linalotuumiza ila hakuna tatizo ni mchezo wetu.

"Hatuna mshambuliaji kamili kwa sasa kutokana na majeruhi yanayowasumbua, mchezaji kama Aiyee (Salim) kwa sasa hayupo sawa ila tumejipanga kufanya vizuri kikubwa sapoti," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic