August 19, 2019


Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Mbelgiji Patrick Aussems, amesema kuwa haoni dalili nzuri ya kufanya vema kwa timu za Tanzania katika michuano ya kimataifa msimu ujao kutokana na ratiba mbovu ya ligi kuingiliana na ile ya CAF.

Mbelgiji huyo ametoa kauli hizo akizilenga timu za Simba na Yanga ambazo zinashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika sambamba na Azam pamoja na KMC ambazo zinaiwakilisha nchi kunako Kombe la Shirikisho.

Kocha huyo aliyeweka rekodi ya aina yake kuifikisha Simba kunako hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, anaamini timu za Tanzania hazitakuwa na nafasi ya kufanya vema tofauti na wengi wanavyotarajia.

"Nisiwe muongo, ratiba ya ligi imekuwa ya ajabu na inashangaza kwa sababu inatoa nafasi finyu kwa wawakilishi wa nchi.

"Katika michuano hii ya kimataifa sioni kama kuna timu Tanzania itaweza kufika kwenye hatua nzuri", amesema Aussems.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic