August 21, 2019


BAADA ya hivi karibuni mabeki wa kati wa Simba, Pascal Wawa na Erasto Nyoni kufanya makosa kadhaa katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC, wachezaji hao jana waliwekwa kitimoto na kocha mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Patrick Aussems.

Aussems amefi kia hatua hiyo ili kuhakikisha wachezaji hao wanajirekebisha kabla ya kupambana na UD Songo ya Msumbiji katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afi rka.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na timu zote zitashuka uwanjani zikiwa na kumbukumbu ya kutofungana katika mchezo wa kwanza uliochezwa huko nchini Msumbiji.

Habari za kuaminika kutoka katika timu hiyo ambazo Championi Jumatano limezipata, zimedai kuwa Aussems alikutana na wachezaji hao baada ya mchezo wao huo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.

“Kuna makosa ambayo walikuwa wakiyafanya katika mchezo ule ambayo kama Azam wangekuwa makini hakika wangefunga mabao mengi.

“Kwa hiyo kutokana na hali hiyo kocha alikutana nao na kuzungumza nao juu ya mapungufu hayo na kuwataka kubadilika na kuongeza umakini zaidi katika mechi yetu ijayo dhidi ya UD Songo,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Alipoulizwa kuhusiana na hilo, Aussems alisema kuwa: “Ni kweli baada ya mechi hiyo nilikutana na wachezaji wote na kuwaambia mapungufu ambayo yalijitokeza katika mchezo huo na nikawakumbusha kuwa makini zaidi. “Hata hivyo, tunaendelea na maandlizi yetu kwa ajili ya mechi yetu ijayo na ni matumaini yetu kuwa kila kitu kitakuwa sawa.”

11 COMMENTS:

  1. Yaani makosa afanye Zimbwe Jr alafu Nyoni ndo awekwe kitimoto?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wote hao wanapaswa kucheza kama kitu kimoja. Lazima kuwe na umoja katika ulinzi. Na hicho ndio kimekosekana kwa sasa. na kwenye viungo wakabaji nao bado kuna shida. Hawatoi msaada kwa wakati.

      Delete
  2. Ukweli beki za kati za Simba, zimekuwa na makosa memgi. Na kama timu pinzani zingekuwa makini hata ile ya UD Songo tungefungwa mengi sana.

    ReplyDelete
  3. Kiuhalisia Nyoni siyo beki bali ni kiungo mkabaji, hata ukioangalia aina ya uchezaji wake ni wa kiungo siyo wa beki,mwaka jana nilidhani alichezeshwa kama beki kwa sababu hatukuwa na mabeki wazuri asilia nikidhani msimu tutasajili mabeki wazuri wa kati ili yeye acheze kama kiuongo mkabaji lakini inaonekana hawakupatikanamabeki wa kati wazuri na hivyo kulazimika kuendelea kumtumia Nyoni.Hivyo Nyoni hastahili lawama bali uongozi wa timu kwa kushindwa kusajili mabeki wazuri wa kati na badala yake kulazimika kumchezesha Nyoni kwenye nafasi ambayo kimsingi hastahili kucheza bali kwa sababu anaewza kucheza namba nyingi,lakini nafasi yake halisi ni ya kiungo mkabaji.Nyoni ni soft sana kuchexa kama beki anacheza mchezo laini sana na anatake risk sana wakati yeye ni mchezaji wa mwisho any risk ina madhara makubwa,beki wa mwisho hapaswi kucheza hivyo kwa kioungo sawa maana akikosea bado kuna mabeki wanaweza kusaidia. Vile vile yeye na Wawa hawatifautiani na hawana speed na wanapenda kupata sana mbele na kuwa vulnerable kwa counter attacks pia siyo wazuri kwa mipira ya juu.Simba bado kuna shida kubwa sana kwenye Central defenders,uongozi haujatafuta dawa tatizo hili sugu ambalo limeonekana bayana tangu msimu uliopita.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeongea vizuri jombaa, shida nyingine ni kuwa Nyoni na Wawa wanacheza aina moja ya uchezaji, hawna speed na maamuzi ya haraka. Ningeshauri yule mbrazil na Wawa wacheze pale nyuma lakini Nyoni asogee kama kiungo mkabaji kama kule AFCON akisaidiwa na Mkude au Muzamiru, Shiboub asogee mbele acheze kama namba tisa akimsaidia Kagere, huku pembeni kushoto acheze Mbaga maana anajua kukaba zaidi kuliko Mohamed ambaye ni mzuri wa kushambulia shida anachelewa kushuka kukaba, kulia kapombe, winga moja awe Deo/MIRAJI na nyingine awe Dilunga/Chama...Hapo hachomoki mtu..

      Delete
  4. Hakuna mabadiliko yeyote yaliyofanyika kwenye beki ya Simba zaidi ya kusema hali imekuwa mbaya zaidi. Ile sare ya kule Msumbiji ni kama ngekewa tu na kutokana na mchecheto wao wenyewe UD Songo ila Simba ilistahili kuadhibiwa vilivyo hata goli nne.Na kama UD Songo watayafanyia kazi makosa yao kule Msumbiji basi hapana shaka uwezekano wa Simba kuondolewa katika hatua ya mwanzo klabu bingwa Africa upo mkubwa. Viongizi ama tuseme kocha wametufelisha wana msimbazi kwenye eneo la ulinzi kwenye timu yaani beki ya Simba hasa beki ya kati ni majanga matupu ni jipu linalosubiri kupasuka kuchefua hali ya hewa.

    ReplyDelete
  5. Nafikiri shida sio Wawa au Nyoni.....shida ni Ausems kukariri binafsi sioni tatizo la Mlipili au Santos kutoaminiwa....Wawa ni tatizo na habadiliki (nafikiri umri) na Nyoni anasumbuliwa na fatique kwani toka ligi iishe hajapumzika.Mkude halikadhalika siamini kama ni bora kuliko Fraga....kocha anakuja na hoja dhaifu ya kutojua lugha wakati mpira una lugha yake.Kukariri nsiko kutakokako mwondoa Ausems pale simba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaani unachofikiria ndio na mimi nilikuwa nakifikiria.. hawa wabrazil hasa mabeki wapo vizuri sioni shida yao sema kocha naona kama hawapendi hawa wabrazili na hawa ndio watakao mwondoa hapo klabuni tukitolewa klabu bingwa jumapili! siku ya Simba day jamaa Santos alicheza vizuri sana. Fraga aliingia second half pia alicheza vizuri pia sasa sijui tatizo ni nini? mbona wawa na nyoni bado wanafanya makosa yale yale toka msimu uliopita????

      Delete
    2. Simba imesajili vizuri kwa msimu huu. Tairone, Kennedy wana physique na height ya kucheza central defence. Fragha na Shiboub wote wana physique na height, pia ni reinforcement nzuri katika mfumo wa double pivot. Kocha ana options nyingi sasa. Mwenye match fitness ndiye apewe nafasi kwenye timu.

      Delete
  6. Kiukweli nyoni na wawa inabidi wapumzishwe waingizwe wale wabrazili wako vizuri shida mwalimu anaonekana ana Mahaba Sana na wawa Mimi binafsi bora angebaki kotei kuliko wawa na Hawa Brazilians mbona wako vizuri mno? Ile mechi ya UD SONGO tulinusurika kwa bahati tu ila centre back ilikuwa inafanya makosa mengi na Huyu shabalala sio Mzuri kwenye kukaba bora gadiely kwa Shomari sioni tatizo kabisa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic