August 22, 2019



SELEMAN Matola, Kocha wa Polisi Tanzania amesema kuwa kikosi chake kimetengamaa na kitaleta ushindani kwenye ligi msimu ujao.

Polisi Tanzania imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu na itakuwa miongoni mwa timu 20 ambazo zitashiriki ligi inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 24 juni ambapo itacheza na Coastal Union ya Tanga uwanja wa Ushirika Moshi.

“Tupo sawa na kikosi chetu kina moto wa kutosha kabla ya ligi kuanza hivyo imani yetu ni kufanya makubwa msimu utakapoanza hasa ukizingatia ni kikosi kipya lazima wachezaji wawe na mambo mapya.

“Kwenye ligi hatuna hofu iwe ni Coastal Union, Simba, Yanga, Azam tutapambana, tunatambua kwamba ligi itakuwa ngumu nasi tutakaza," amesema.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic