August 22, 2019


WAKATI kikosi cha Yanga kikitarajia kushuka uwanjani Jumamosi ya wiki hii huko nchini Botswana, safu ya ulinzi ya timu hiyo imetajwa kuwa ndiyo itakayokuwa bora zaidi msimu huu kwa timu za Ligi Kuu Bara.

Yanga itapambana na Township Rollers ya Botswana, Jumamosi hii katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ukiwa ni wa marudiano baada ya ule wa kwanza kuchezwa hapa nchini na timu hizo kufungana bao 1-1.

Akizungumza na Championi Jumatano, aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Mrundi Amissi Tambwe, amesema kuwa safu ya ulinzi ya Yanga ndiyo inayoonekana kuwa bora zaidi kuliko ile ya Simba.

Alisema katika mechi ya kirafi ki ambayo Yanga ilicheza na AFC Leopards ya Kenya, safu ya ulinzi ya timu hiyo iliyokuwa ikiundwa na Kelvin Yondani, Lamine Moro, Ally Sonso na Paul Godfrey ‘Boxer’ ilionekana kuwa bora zaidi na ngumu kupitika ukilinganisha na msimu uliopita.

“Kutokana na hali hiyo naamini kabisa safari hii Yanga ina ukuta imara zaidi ukilinganisha na timu nyingine za ligi kuu ambazo nimebahatika kuona mechi zao. “Haswahaswa uwepo wa Yondani pamoja na Sonso ambao nawajua vizuri uwezo wao, unaifanya timu hiyo kuwa na ukuta imara,” alisema Tambwe.

Akizungumzia safu ya ushambuliaji ya Yanga, alisema kuwa: “Washambuliaji waliopo ni wazuri ila wanatakiwa kujiongeza wenyewe kuhakikisha wanakuwa fi ti, wakisema wamtegemee kocha awabadilishe, watafeli. “Nasema hivyo kwa sababu naijua vizuri aina ya ufundishaji ya kocha huyo.”

CHANZO: CHAMPIONI

2 COMMENTS:

  1. Tambwe uko sahihi, Zahera ni kocha mzuri kwa mabeki tu. Kwa ushambuliaji mpaka wachezaji wajitambue wenyewe tu.

    ReplyDelete
  2. Tambwe usivunjike moyo endelwa kusifu huenda wakakuonea huruma na kukurejesha dirisha dogo lijalo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic