August 19, 2019


Straika wa Yanga kutoka Burundi, Amis Tambwe, amefunguka kwa kusema kuwa amefurahishwa na nafasi ya ushambuliaji ya Simba kufuatia ushindi waliopata katika mechi ya Ngao ya Jamii kwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-2.

Tambwe ambaye aliwahi pia kuichezea Simba miaka kadhaa iliyopita, amesema Simba wameimarika zaidi kunako eneo la ushambuliaji jambo ambalo limemfanya afunguke na kutoa pongezi hizo.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ulishuhudiwa mabao yakiwekwa kimiani na Sharaf Shiboub aliyeingia kambani mara mbili sambamba na Clatous Chama aliyefunga moja huku Francis Kahata naye akifunga moja.

"Kusema ukweli safu ya ushambuliaji ya Simba imekuwa vizuri hivi sasa tofauti na msimu uliopita.

"Kusajiliwa kwa Deo Kanda na Kahata kumezidi kutia morali na makali mbele na uwepo wa Shiboub umesaidia kuwasaidia washambuliaji wanaofanya kazi ya kufunga", amesema.

Mbali na kusifia, Tambwe pia amefunguka kwa kuikosa nafasi ya ulinzi akisema bado ina mapungufu.

"Kwenye safu ya ushambuliaji bado kuna matatizo yaleyale ambayo yaliigharimu timu msimu uliopita haswa kwa mechi za nyumbani na ugenini.

"Kwa maana hiyo wakikutana na washambuliaji wazuri wanaojua zaidi itakuwa ngumu kwao kuwazuia na makosa ya msimu uliopita yatazidi kujitokeza.

"Namuomba Kocha alifanyie kazi suala hilo ili kuhakikisha Simba inakuwa fiti kila idara".

7 COMMENTS:

  1. Kwa kiasi fulani kocha wa Simba kama vile hana washauri au wanaomshauri wanaogopa kumwambia ukweli kwani tatizo la beki ya Simba ni donda ndugu hivi sasa.Inashangaza sana kuona kocha aking'ang'ania beki ile iliyoigharimu timu msimu uliopita. Kocha hata kwenye mechi za kirafiki anashindwa kuwatimzama mabeki wengine wana uwezo gani? Kwakweli kuelekea klabu bingwa Africa ni mashaka mtupu kwenye eneo la beki ya simba Tambwe yupo sahihi kabisa.

    ReplyDelete
  2. Beki ya simba ni uchochoro tusubiri yatufike wala tusijelalamikiana.. maana wanaambiwa hawaelewi. wawa atatugharimu simba wangemtumia mbrazil. kama walikuwa wanajua wabrazil lugha walikuwa wanawasajili wa nn? kwanza uwanjani hatufanyi mitihani ni mpira tuu.. sisi tumesema wasipofanyia kazi shauri yao.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usiseme beki ya Simba... Sema Zimbwe Jr ni uchochoro.. Yeye pekee ndo anaigharimu timu.. Kama vipi kocha ambadilishe namba acheze 11 badala nafasi anayocheza sasa!! Ni mzigo kwa mabeki wenzake!

      Delete
  3. Kabisa Kocha wa Simba ni binaadamu mwenye mchecheto ni sawa na askari aliekabidhiwa silaha akawa ana babaika jinsi za kuzitumia. Kama lugha ni tatizo kati ya mbrazili na wawa au mbrazili na Erasto Nyoni kwanini asiwachezeshe wabrazili wote kwa pamoja beki tano na nne? Kwani yule mmoja tubaambiwa ni kiraka na anapiga senta half bila ya shaka yeyote.

    ReplyDelete
  4. Nilikuwa nahisi matatizo haya nayaona peke yangu. Yaani ni juzi tumetoka kupata humiliation ya goli tano tano lakini hatuoni improvement. We are doing the same mistakes over and over again. Dynamos, Songo na Azam wameonesha mapungufu ya defence yetu. Kufungwa ni kawaida ila namna unavyofungwa ndio inafedhehesha. Bado hatuna uwezo wa kucheza mipira ya set pieces langoni kwetu na tunawaachia fowadi wa timu pinzani kuliona lango wazi wazi hakuna mtu anaeenda kufanya blocking. Nakumbuka zama za akina Masatu na Pawasa.

    ReplyDelete
  5. Ni kweli kabisa saf ulizi cocha inambid watumie wablazili wanaweza wakawa wazuri kuliko wawa, wawa kimataifa hawezi kabisa

    ReplyDelete
  6. Nimeshangaa kuona kocha anaendelea kupanga safu ya ulinzi ile ile iliyotugharimu msimu uliopita licha ya kufanya usajili wa kuboresha kikosi. Ukiondoa Kapombe ambaye hakuwepo kwenye vile vipigo vya 5 - 0 safu ya ulinzi anayoiamini kocha ni ile ile na hakuna improvement yoyote kiuchezaji. Mabeki hawajui kujipanga kwenye krosi na bado wanaruhusu washambuliaji wa timu pinzani kupiga mashuti karibu na lango lao bila bughudha yoyote. Kocha ajaribu combination tofauti ya mabeki. Kama Wabrazil bado amrejeshe hata Mlipili pale kati. Nilidhani sehemu ya ulinzi ndio ilikuwa muhimu zaidi kuongeza wachezaji wenye ubora.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic