August 21, 2019


MKUFUNZI wa timu ya soka upande wa akina dada nchini England, Phil Neville, amesema kuwa wachezaji wanapaswa kususia mitandao ya kijamii ili kutuma ujumbe mzito kwamba ubaguzi wa rangi hautakubaliwa.

Matamshi ya Neville yanajiri baada ya kiungo wa kati wa Manchester United, Paul Pogba, kupokea machapisho ya ubaguzi wa rangi mitandaoni kufuatIA hatua yake ya kukosa penalti wakati wa mechi iliYotoka sare ya 1-1 dhidi ya Wolves siku ya Jumatatu.

”Lazima tuchukue hatua mwafaka sasa kama jamii ya kandanda. Tumeona, na wachezaji wangu katika mitandao ya kijamii, ligi ya Premiere na mabingwa wameona,” alisema Neville.

”Sijui kama jamii ya soka tunafaa kususia mitandao ya kijamii, kwa sababu Twitter haitachukua hatua yoyote, Instagram haitafanya lolote – wanakutumia barua pepe wakisema kwamba watachunguza lakini hakuna kinachofanyika.

”Nimepoteza imani na yeyote anayeendesha idara za mitandao hii, hivyo basi tutume ujumbe mzito. Tususie mitandao ya kijamii kwa miezi sita. Tuone athari yake kwa kampuni hizo za mitandao ya kijamii,” alisema.

Siku ya Jumanne, Twitter ilitoa taarifa ikisema kuwa inashutumu kwa nguvu matusi na sasa imepiga marufuku baadhi ya akaunti kwa kukiuka sera yake ya chuki. Iliongezea: Tunajua kinachoendelea kuhusu ubaguzi wa rangi mitandaoni dhidi ya wachezaji fulani nchini Uingereza katika siku za hivi karibuni.

Tunachunguza matamshi hayo na tutaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya akaunti yoyote inayokiuka sheria. Hili ni swula la kijamii na linahitaji jamii kuchukua hatua. Hii ndiyo sababu tunaendelea na mjadala na muungano wa wachezaji wa kulipwa pamoja na ‘kick it out’ na wako tayari kushirikiana kutatua matusi mitandaoni na tabia za kibaguzi katika sekta hii.

Taarifa kutoka Facebook ilisema: Hakuna nafasi ya ubaguzi ama tabia ya matusi katika Instagram na tunawekeza pakubwa katika kuimarisha vifaa na teknolojia ili kuzuia uonevu na unyanyasaji. Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walianzisha kampeni ya #istandwithpogba

Watu ambao huvunja maelekezo yetu watapigwa marufuku kutumia Instagram. Wachezaji wenza wa Pogba wamekosoa matusi hayo dhidi ya raia huyo wa Ufaransa ambaye penalti yake ya dakika ya 68 iliokolewa na kipa wa Wolves Rui Patricio – ikiwa ni penalti ya nne iliyopotezwa na mchezaji huyo akiichezea United katika ligi ya Premiere tangu msimu uliopita. Harry Maguire alitaka kampuni za mitandao ya kijamii kusitisha kujifanya kwamba zina huruma huku Marcus Rashford akisema kwamba inatosha na suala hilo linafaa kukomeshwa.

”Manchester United ni familia. Pogba ni mwanachama wa familia, unapomshambulia mnatushambulia sisi sote”, mshambuliaji huyo wa England aliongezea katika mtandao wa Twitter. United imesema kwamba inatumia kila mbinu kuwafichua wale waliomtusi Pogba.

Watu waliowasilsha maono hayo hawaungi mkono maadili na thamani ya klabu yetu na inatupa moyo kuona kwamba idadi kubwa ya mashabiki wetu wameshutumu hilo katika mitandao ya kijamii, ilisema taarifa ya United. ‘

‘Tutafanya kazi ya  kuwabaini watu wachache waliohusika katika visa hivi na kuchukua hatua kali. Tunazitaka kampuni za mitandao ya kijamii kuchukua hatua dhidi ya kesi kama hizi,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic