August 21, 2019


TUMEWATIBULIA! Hivyo ndivyo viongozi wa Yanga wanatamba ni baada ya kushtukia janja ya wapinzani wao Township Rollers ya nchini Botswana.

Yanga inatarajiwa kuvaana na Rollers Jumamosi hii kwenye mji wa Gaborone huko Botswana katika mchezo wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu hizo katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema kuwa timu inafanya mazoezi saa tisa kamili alasiri baada ya benchi la ufundi la timu hiyo kushauriana na viongozi.

Mwakalebela alisema kuwa lengo ni kuzoea mazingira ya jua kali ili wachezaji wazoee kutokana na aina ya uwanja wa bandia watakaoutumia katika mchezo huo.

 “Kila mtu anafahamu mazingira ya uwanja wa nyasi bandia, siku zote unashika joto kwa sababu ya jua kali linalopiga uwanjani hapo.

“Hivyo, ili wachezaji wetu wazoee mazingira hayo benchi la ufundi kwa kushirikiana na viongozi tumeshauriana kufanya mazoezi saa tisa alasiri.

“Muda huo ni sahihi kwetu, tukiamini wachezaji watozoea mazingira hayo ya uwanja, tunafahamu wenzetu wameshauzoea uwanja huo wa nyasi za bandia,”alisema Mwakalebela.

Yanga wanatakiwa kupata ushindi au sare ya zaidi ya bao 1-1 ili kuweza kufuzu kwa hatua ya kwanza ya michuano hiyo mikubwa Afrika.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic