February 21, 2020



KIKOSI cha Azam FC kimeanza maandalizi ya kuiwinda Namungo FC kwa ajili ya mchezo wao utakaopigwa kesho, Februari 22, saa 10:00 Uwanja wa Majaliwa.

Azam FC iliyo chini ya Arstica Ciaoba itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kugawana pointi moja na Ndanda FC baada ya kupata sare ya kufungana bao 1-1 mchezo uliochezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Ndanda ilianza kucheka na nyavu kupitia kwa Vitalis Maynga kipindi cha kwanza na Andrew Simchimba alipindua meza kipindi cha pili kwa Azam FC.

Ofsia Habari wa Azam FC,Jaffar Maganga amesema kuwa kila kitu kipo sawa wanaamini watapata pointi tatu muhimu.

"Maandalizi yapo vizuri na wachezaji wana morali, kikubwa ni kuona namna gani watafanya uwanjani kile ambacho wameelekezwa na mwalimu," amesema.

Azam FC ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 45 baada ya kucheza mechi 23.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic