February 21, 2020


OMARY Madenge, Kocha Msaidizi wa Biashara United amesema kuwa mpango mkubwa kwa timu yake ni kupambana mbele ya Simba na kupata pointi tatu bila kuhofia makali ya washambuliaji wa wapinzani wake.

Biashara United ya Mara, itashuka Uwanja wa Taifa kesho kumalizana na Simba mchezo wa pili ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa mabao 2-0.

Madenge amesema:"Tupo tayari kupambana mbele ya safu yao ya ushambuliaji inayoongozwa na Meddie Kagere, tunajua uimara wao ulipojificha nasi hatuna mashaka tupo vizuri, mashabiki watupe sapoti,".

Biashara United ipo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 32 kibindoni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic