February 21, 2020

NAHODHA wa Simba, John Bocco amesema kuwa kesho watambana mbele ya Biashara United ili kupata pointi tatu muhimu.

Simba itaikaribisha Biashara United, Februari 22, Uwanja wa Taifa mchezo wa ligi wa pili kwa mzunguko wa pili.

Bocco amesema: "Ni mchezo wetu mgumu kutokana na ushindani uliopo, tunawaheshimu wapinzani wetu kwani ni timu nzuri ambayo tutakutana nayo ila nasi pia tupo vizuri tutapambana ili kupaya pointi tatu muhimu mashabiki watupe sapoti," amesema.

Bocco ana mabao matatu ndani ya ligi kwa msimu huu wa 2019/20 na pasi moja ya bao.

4 COMMENTS:

  1. Boko kiongozi na sasa anaonekana kuwa yupo vizuri.Ujumbe wangu kwake ni kwamba kama kiongozi wanatakiwa kutulia zaidi wanapofika golini. Kama kiongozi wanatakiwa kuwa na mawasiliano mazuri wanapofika golini kwani tumeona mara nyingi mchezaji analazimisha kufunga wakati kuna mchezaji mwenzie alie kaa pazuri zaidi. Ligi hii haina cha timu ndogo ukizubaa unaadhirika. Kitu kimoja Simba wameshindwa kujifunza kutoka klabu bingwa Africa ambacho kama wangejifunza vyema Simba wasingepata taabu kwenye ligi kuu. Kitu hicho sio kingine bali ni presha ya timu mwenyeji kwa mgeni au timu presha ya timu kubwa kwa timu ndogo. Simba ilipigwa tano na vita klabu sio kuwa walikuwa wabovu bali ni gemu plan ya maximum presha kwa timu ngeni kutoka kwa vita club. Simba Walipigwa tena tano na Alhaly ya Egypt kwa staili ile ile ya vita club ya kuwekea pressure ya nguvu baada kuanza tu kwa mchezo. Simba wakaja kupigwa nne 4-1 na TP Mazembe kwa staili ile ile ya pressure.Mechi zote hizi John Boko ndie aliekuwa kapteni na ikiwa mimi shabiki bado nina kumbu kumbu nzuri sasa kwanini kapteni asahau? Timu kama biashara,Simba wakikumbuka mateso ya vita club au Tp Mazembe na wachezaji kuyafanyia kazi kwa vitendo basi sioni nafasi ya biashara kuisumbua Simba. Wakati mwengine wachezaji wetu wanajilemaza wao wenyewe bana! ila kwa Simba hii ni timu yenye uzoefu wa mechi za hatari na ni wakati wao sasa wa kuonesha utofauti.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivyo vipigo vya caf champions league bado hatujajifunza. Hata ligi kuu, unaona defence haichezi vizuri na midfield ya chini. Mabeki wanaokoa mipira ya juu ya hatari lakini haifiki mbali na lango unategemea midfielders waje kufanya kuokoa lakini wanachelewa.

      Delete
  2. Unajua kila mtu ana mawazo yake, lakini kuna mtu anakwambia kitu na unaona yes! apa kuna logic. Aliye comment hapo juu jamaa anaenda mpirani na macho yote. nakubali hatuingii mashindanoni na tukarudi tumejifunza kitu, Kama tunataka kupiga hatua kila tukirudi tuone kitu gani tumejifunza mara ya mwisho na kukifanyia kazi. Nakubali hicho ndio tunacho kikosa na ni muhimu ili kupiga hatua mbele.

    ReplyDelete
  3. Pambaneni pote sio huko tu mechi zote mnapenda kucheza mchezo wa kuridhika sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic