February 21, 2020


MZAMIRU Yassin, kiungo wa Simba ameanza mazoezi ili kurejea uwanjani kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye mechi dhidi ya Yanga.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Januari 4 timu zote zilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.

Yassin akiwa na Simba kwenye mechi za Ligi Kuu Bara alihusika kwenye jumla ya pasi tatu za mabao ambapo mbili alimpa Meddie Kagere mwenye mabao 13 na moja alimpa Miraj Athuman mwenye mabao sita.


4 COMMENTS:

  1. Tulikukosa kwenye mechi nyingi Mzamiru karibu sana.

    ReplyDelete
  2. Muzamiru yupo fiti kimwili ila Kuna vitu anakosa kwa nafasi anaocheza sasa.sote hatuwezi kuwa makocha au wataalam wa akili ila kutoa ushauri kwa nia ya kutaka kuona mwenzako anafanikiwa nadhani ni jambo jema. Kwanza kabisa sina hakika kama Muzamiru anapangwa namba sahihi ndani ya Simba au analazimishwa kupangwa namba kwa mahitaji ya timu na si kwa ufanisi wa mchezaji? Muzamiru mara nyingi ndani ya simba hupangwa kama kiungo mkabaji ila hata kwa jicho la jongoo unaona kabisa kuwa Muzamiru ni kiungo mshambuliaji hata ikibidi kuwa mshambuliaji basi anaweza kukupa unachokitaka kwa ubora ulio na thamani zaidi kuliko kuwa kiungo mkabaji na hii ni kazi ya Matola kumuongoza Sven katika kujua tabia za wachezaji wazawa ili watumike kwa mafanikio na ije kuwa msaada kwa Taifa. Muzamiru kama ni kiungo mkabaji basi kwanza anatikiwa kubadilisha tabia kwani ni mpole mno kuwa kiungo mkabaji na si ajabu watu kumshushia lawama kwenye mechi ya simba na Yanga alipompendezesha mapinduzi balama na kufunga bao jepesi kiasi cha kutia kichefuchefu kwa kiungo fundi kama yeye mwenye uzoefu mkubwa wa mechi za kimataifa kuja kufanya makosa kama yale. Kama muzamiru anataka kuwa kiungo mkabaji wa ukweli basi amuangalie tu Fabnho wa Liverpool au Cacemiro wa real Madrid au hata Ngolo kante. Hawa watu watamtosha Muzamiru kujua kuwa kiungo mkabaji sio sehemu ya siasa ni utendaji tu wenye maamuzi magumu. Anatakiwa pia kuwa very aggressive kunako kumiliki eneo lake la kazi yaani eneo la kiungo. Kwa imani yangu kama Muzamiru atapata maelekezo sahihi ni moja ya wachezaji tunaowahitaji sana kwemye timu yetu ya Taifa kwani wabunge walipokwenda Egypt kuiunga mkono Taifa stars walisikika wakilalamika kuwa vijana wetu wanakosa miili ya kazi. Kuna wale wenye kuleta siasa kwenye michezo waliwashutumu wabunge kwa kuleta zarau ila kwa tunaopenda kusikia ukweli tuliwapa kongole wabunge wakiongozwa na ndugu Ngugai kwani ukweli ni kwamba vijana wetu hawapo fiti kulinganisha ugumu wa kazi yao. Kama mchezaji yupo fiti kimwili basi ni rahisi kumuweka sawa kiakili kwa mapambano. Kuna jitihada zimefanyika sio siri kwa baadhi ya timu kuwapandisha madaraja ya kiutimamu wa mwili wachezaji wao. Timu kama Azam, na hasa Simba wachezaji wao wengi wapo vizuri kimwili na kama kujilegeza basi ni maamuzi yao wao wenyewe binafsi ila kwa macho ya uwazi kabisa unaona wachezaji wa Simba wapo timamu kiasi na si kwa bahati mbaya ila wanawataalamu maalum pale kwa ajili kuwajenga miili na ingekuwa vizuri kila timu ikawa na wataalam wa lishe na mazoezi ya viungo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huu ndio uchambuzi ingawa amelazimika kuandika kirefu kuelewesha.

      Delete
  3. Muzamiru ni defensive midfielder mwenye uwezo wa kushambulia pia. Muhimu sana ndani ya Simba.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic